Jumatano, 17 Julai 2019

Ebola Goma



Ebola Goma

Shirika la Afya Duniani(WHO) litafanya kikao cha dharula hii leo kutathmini hatari ya Ebola nchini Congo.

Mkutano huu unafanyika siku moja, baada ya kifo cha kasisi mmoja aliyefariki baada ya kusafiri Butembo kufanya maombi.

Taarifa inasema mhubiri huyu alizuru eneo la Butembo ambalo ni baadhi ya maeneo yanayokabiliwa na ugonjwa wa Ebola kwa muda.

Katika shughuli zake za maombi aliguza wagonjwa na huenda hapo ndipo alipoabukizwa maradhi hayo makali.

Alirudi Goma huku anaumwa na punde alipoenda kutafuta matibabu kwenye zahanati ,akapatikana na ugonjwa wa Ebola.

Moja kwa moja wataalamu wa afya wakachukua hatua kumsafirisha moja kwa moja hadi Butembo kupokea matibabu ya dharula, lakini kwa bahati mbaya akafariki.

Goma ni mji ulio na idadi ya watu milioni moja ,kwenye pwani ya Ziwa Kivu, karibu na Rwanda. 

Ni mara ya kwanza ugonjwa huu kuripotiwa Goma huku wasiwasi ukitanda katika nchi jirani ya Rwanda.Kuna shughuli nyingi hufanyika kila siku mpakani ,hasa katika mji wa Gishenyi.

Serikali ya Rwanda imesema itakuwa hatua ya dharula mpakani kwa kutoa tahadhari kwa  wananchi wake ili kuepuka kupata ugonjwa wa Ebola.

Mkutano wa leo unatarajiwa kutoa hatua au mikakati itakayofuatwa kuukabili ugonjwa wa Ebola ambao ni tishio nchini Congo na pia nchi Jirani.

WHO inafanya kikao baada ya Mkurugenzi Mkuu , Dkt Ghebreyasus kuzuru Congo kufuatia mripuko wa Ebola katika maeneo ya Butembo na Katwa.

Kwenye taarifa,Dkt Ghebreyesus alitoa hakikisho kuwa Shirika lake litajitahidi kuhakikisha kuwa ugonjwa wa Ebola umekabiliwa.

Takribani wahudhumu wa afya elfu tatu,3000 wamepata chanjo ya Ebola huko Goma.

Zaidi ya watu 1650 wamefariki kutokana na maabuziki ya mapya,huku waabukizi 12 yakiripotiwa kila siku.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni