Shirika la Afya Duniani (WHO) limependekeza dawa ya
Dolutegravir(DTG) katika mapambano yake dhidi ya virusi vya Ukimwi,licha ya
dawa hiyo kushukiwa kuwa na madhara kwa akina mama waja wazito.
Pendekezo hili limetolewa siku mmoja baadaya ya shirika hilo ,kuchapisha
taarifa inayoonyesha kuwa mapambano
dhidi ya Virusi Vya Ukimwi bado yanaendelea.
WHO inapendekeza matumizi ya
Dolutegravir(DTG) kama njia ya kwanza na ya pili ya matibabu kwa watu wote,wakiwemo akina mama wajawazito na pia wenye uwezo wakupata
ujauzito.
Tafiti za awali, zilitia shaka uwezekano wa kuwepo kwa uhusiano kati ya dawa
ya DTG na tatizo linalosababisha watoto
kuzaliwa na tundu kwenye uti wa mgongo na ubongo,yaani Spinal bifida.
Tatizo hili hutokea punde tu mama anapopata
ujauzito huku akitumia dawa ya DTG.
Kenya ni miongoni mwa nchi ambazo zilitoa tahadhari dhidi ya matumizi ya
dawa ya DTG baadaya ya utafiti uliofanywa nchini Botswana kuonyesha kuwa dawa
hiyo ilikuwa na madhara kwa wanawake wajawazito,mwaka uliopita.
Utafiti ulibaini visa vinne vya matatizo hayo kati ya wanawake 426
ambao walipata ujauzito wakati wakitumia dawa hizo za DTG.
Kufuatia utafiti huo,Kenya na nchi
nyingi ziliwashauri wanawake wajawazito na wanawake wanao tarajia kubeba
ujauzito, kumeza dawa za efavirenz (EFV) badala ya DTG.
Hata hivyo ,baada ya majaribio ya
kisayansi ya kuchunguza ufanisi na usalama kati ya DTG na EFV barani Afrika,
sasa ni dhahiri kuwa kiwango cha hatari
ya kupata tatizo la uti wa mgongo na ubongo ni ndogo mno kinyume na ilivyokuwa imekadiriwa hapo awali.
Shirika la Afya Duniani ,inasema kuwa DTG ni dawa ambazo zina ufanisi
zaidi, rahisi kumeza na zina madhara machache kuliko dawa zingine ambazo
zinatumika kwa sasa.
Katika harakati za kupambana na VVU, nchi zinazo endelea 82 ziliripoti kurudia matibabu ya VVU yanayotumia
DTG.
WHO inatia mkazo mapendekezo mapya yaliyoboreshwa na yanayolenga kusaidia nchi zaidi
kuboresha sera za afya.
Kufuatia hayo,WHO imeandaa kikundi cha ushauri wa wanawake wanaoishi
na VVU kutoka katika Nyanja mbalimbali ili kutoa ushauri katika masuala ya sera
zinazohusiana na afya zao, na zile za afya
ya uzazi.
DTG
ilipendekezwa mnamo Juni 2017 kama dawa mbadala ya wanaougua Ukimwi na ambao
hawakupata matokeo mema kwa kutumia dawa ya Efavirenz au zile za ARV.
Kenya ilikuwa nchi ya kwanza barani Afrika kutumia dawa ya Dolutegravir(DTG).
Kenya ilikuwa nchi ya kwanza barani Afrika kutumia dawa ya Dolutegravir(DTG).
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni