Jumatano, 17 Julai 2019

chanjo ya polio(polio vaccine)


Maisha ya watoto milioni ishirini yako hatarini kufuatia taarifa za umoja wa mataifa kuwa watoto hawakupata chanjo dhidi ya magonjwa yanayozuilika mwaka wa 2018.

Magonjwa yanayozuilika ni kama vile,ugonjwa wa kupooza surua,Dondakoo na pepo punda.

Takwimu hizi zimetolewa na  shirika la afya dudniani(WHO) kwa ushirikiano na Shirika la watoto duniani (UNICEF).

Huku chanjo asilimia 86% ikitolewa kuokoa maisha ya watoto,bado kiwango kinachotakiwa cha asilimia 95% duniani kote hakijafikiwa.

Tangazo hili la umoja wamataifa linatia hofu huku ikifahamika kuwa mlipuko Zaidi waweza kutokea endapo hali hii haita shughulikiwa ipasavyo.

Shabaha ya kutoa chanjo ni kuimarisha afya ya watoto na kuepusha hatari ya milipuko ya wagonjwa yanayozuilika.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, Bwana Tedros Adhanom Ghebreyesus amesisitiza kuwa huduma ya chanjo ni muhimu ili kuzuia milipuko ya magonjwa.

Kiwango cha chanjo kwa watoto wasiopata chanjo hasa ni kutokana na hali ya ukimbizi inayosababishwa na vita nchini mwao.

Nchi hizi ni Afghanistan,Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR,Chad, Congo DRC, Ethiopia, Haiti, Mali, Iraq, Niger, Nigeria, Pakistan, Somalia, Sudan Kusini, Syria na Yemen.

Matokeo haya yanaabatana na hali ilivyo nchini Kenya kuhusiana na chanjo ya ugonjwa wa kupooza na chanjo zingine.Inadaiwa kuna kuna upungufu au ukosefu wa chanjo  hospitalini hasa za umma.

Kumekuwa na tuhuma kuwa wazazi wanalazimika kulipa shilingi elfu nane hadi kumi na mbili katika hospitali za kibinafsi ili watoto wao wapate chanjo wanapozaliwa.

Mtoto anapozaliwa anahija kupewa chajo ya kupooza.Chanjo hii hupewa mtoto kupitia kwa mdomo, dozi tatu, halafu baadaye anadungwa shindano anapotimiza miaka mitatu na nusu.

Kinaya ni kuwa Kenya imekuwa katika mstari wa mbele kufanya kampeni dhidi ya chanjo ya ugonjwa wa kupooza (Polio) katika maeneo tofauti nchini.

Zaidi ya hayo,kampeni nyingine ya Polio inatarajiwa kufanyika katika sehemu kadha,huku watoto 2.6 millioni walio chini ya miaka mitano wakitarajiwa kupata chanjo.

Majimbo yaliolengwa katika kampeini ya chanjo ya Polio ni  Mombasa,Tana River,Lamu,Kilifi,Isiolo,Turkana ,Nairobi,Wajir,Garissa na Mandela.

Mwaka 2018 idadi ya watoto walioshambuliwa kwa ugonjwa wa Surua ilikuwa ni 350,000
Kiwango hiki ni mara mbili ya idadi ya watoto walioshambuliwa katika kipindi cha kwa mwaka 2017.

Henrietta Fore Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF, anasema, kuna haja kwa Jumuiya ya Kimataifa kujizatiti vilivyo kutoa chanjo ya kinga kwa kila mtoto duniani.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni