Augmentin bandia
Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya dhidi ya matumizi ya dawa bandia ijulikanayo kama Augmentin,nchini Kenya na Uganda. Shirika hilo limetoa tahadhari wakati kukiwa na ongezeko la ununuzi wa dawa bila ushauri wa wataalam wa afya nchini Kenya. WHO imewataka wakenya wawe waangalifu dhidi ya dawa hiyo bandia ya (antibiotic) inayoamikika kuuziwa wagonjwa katika sehemu mbalimbali za nchi. Augmentin,ni dawa ambayo hutumika dhidi ya maambukizi ya vidudu mwilini na imeorodheshwa na WHO kama mojawapo ya dawa muhimi na inapatikana kwa urahisi katika maduka ya dawa. Kwenye taarifa yake kwa umma, WHO imesema dawa bandia ina muonekano unaokaribiana sana na dawa halisi inayotengenezwa na kampuni ya madawa ya GlaxoSmithKline (GSK). Dawa hizo bandia zilibainika baada ya utafiti wa kukagua ubora wa dawa za antibiotic zinazouzwa kwa wagonjwa. Baada ya vipimo kwenye maabara za kudhibiti ubora ilibainika kuwa baadhi ya dawa ya Augumentin hazikuwa na viungo muhimu...