Jumanne, 6 Agosti 2019

Dkt. Sobbie Mulindi aaga dunia


Dkt. Sobbie Mulindi
Saratani imepokonya nchi ya Kenya Mtafiti wa Virusi Vya Ukimwi na mhadhiri mwandamizi katika idara ya magonjwa ya akili ya Chuo Kikuu cha Nairobi,Dkt Sobbie Mulindi.

Hadi kifo chake hiyo jana,Dkt. Mulindi alikuwa mashuhuri katika janja ya afya.

Ustadi na ukakamavu wake wa utafiti na elimu ya kupunguza maambukizi ya VVU/IKIMWI ulijulikana sio Kenya tu lakini Afrika na dunia yote kwa jumla.

 Pia Mulindi alikuwa Naibu Mkurugenzi wa zamani wa Baraza la Udhibiti wa Ukimwi la Taifa (2008-2014)
Dk Sobbie Z. A. Mulindi alianza masomo yake katika Chuo Kikuu cha Nairobi, na baadaya akawa mkufunzi kwenye chuo hiko.

Zaidi ya hayo,alitumika katika hospitali kuu ya Kenyatta na katika Hospitali ya wagonjwa wa kiakili ya Mathari kufuatia uzoefu kwake katika nyanja ya wagonjwa na kiakili yaani maswala ya kisaikolojia.

Amekuwa mhadhiri katika chuo cha Nairobi kwa zaidi ya miaka 30

Isitoshe,alishiriki katika kukuza Mikakati ya Kitaifa ya kuzuia VVU / UKIMWI nchini Kenya na nchi zingine ikijumuisha Afrika Kusini, Swaziland, Rwanda, Benin, Somali, Kongo  Brazzaville.

Alishiriki kikamilifu kuwapa ushauri wahanga wa milipuko kama vile Bomu jijini Nairobi ,uliotokea Agosti 7, 1998, na mashambilishi ya kigaidi ya Westgate ya mwaka wa 2013.

Pia aliongoza Timu za Ushauri wa Matibabu kwa waadhiriwa wa ajari za ndege ya Kenya huko Abidjan Cote d'Ivoire mwaka wa  2000 na ile ya Duala Cameroon mwaka wa  2007.

Alipokuwa  Mkurugenzi mratibu wa mipango  ya VVU na UKIMWI,alifanya juhudi  ili kupunguza maambukizi kutoka asilimia 14 hadi asilimia 5.6 hivi sasa.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni