Alhamisi, 29 Agosti 2019

Augmentin bandia

Image result for augmentin
Shirika la Afya Duniani (WHO) limeonya dhidi ya matumizi ya dawa bandia ijulikanayo kama  Augmentin,nchini Kenya na Uganda.
Shirika hilo limetoa tahadhari wakati kukiwa na ongezeko la ununuzi wa dawa bila ushauri wa wataalam wa afya nchini Kenya.
 WHO imewataka wakenya wawe waangalifu dhidi ya dawa hiyo bandia ya (antibiotic) inayoamikika kuuziwa wagonjwa katika sehemu mbalimbali za nchi.
Augmentin,ni dawa ambayo hutumika dhidi ya maambukizi ya vidudu mwilini na imeorodheshwa na WHO kama mojawapo ya dawa muhimi na inapatikana kwa urahisi katika maduka ya dawa.
Kwenye taarifa yake kwa umma, WHO imesema dawa bandia ina muonekano unaokaribiana sana na dawa halisi inayotengenezwa na kampuni ya madawa ya GlaxoSmithKline (GSK).
Dawa hizo bandia zilibainika baada ya  utafiti wa kukagua ubora wa dawa za antibiotic zinazouzwa kwa wagonjwa.
Baada ya vipimo kwenye maabara za kudhibiti ubora ilibainika kuwa baadhi ya dawa ya Augumentin hazikuwa na viungo muhimu vinavyohitajika na vilivyo kwemye mifuko yake ya upakiaji na pia mandishi.
Dawa bandia zinaweza kusababisha madhara makubwa mwilini,ingawa hadi kwa sasa hakuna aliyeipoti hayo,ingawa kuna wale wanaweza kuwa wameona mabadiliko wanapotumia dawa hii nawasijue ni madhara ya dawa bandia.
Serikali ya Kenya kwa muda mrefu imewaonya wananchi dhidi ya kununua dawa kwa maduka ya dawa bila kibali za daktari.Pia kuna maduka ya madawa yaliyopigwa marufuku kwa kuuza madawa bila lesheni,huku ikiaminika huwa wanauza dawa bila ujuzi elimu  unaostahili kutekeleza majukumu haya.
Hii ni mara ya mbili tahadhari dhidi ya dawa hii kutolewa na WHO barani Afrika.
Tahadhari ya kwanza juu ya uwepo wa dawa hizo bandia ilitolewa mwanzoni wa mwaka huu 2019.
Kampuni ya madawa ya GlaxoSmithKline imesema haihusiki kwenye utengenezaji wa   dawa hizo bandia

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni