Jumatatu, 18 Mei 2020


Shirika la Afyan duniani linafanya kikao hii leo mjini Geneva kujadili maswala ya COVID 19

Mkutano huu wa siku mbili unaendelea huku Taiwan ikipinga hatua ya kutengwa katika vikao vya baraza la shirika la afya duniani WHO huku ikisema itakuwa ni hasara kutohudhuria kikao hiki ikizingatiwa kuwa imefanikisha juhudi zake za kukabiliana na virusi vya Corona.

Taiwan na nchi nyingine kadhaa zimelitaka shirika hilo kuialika katika mkutano huo unaofanyika moja kwa moja kupitia mitandao.

Haya yanajili huku uhusiano baina ya Uchina na marekani ukiendelea kuzorota.

Hapo awali Marekani ambaye ni muhisani mkuu wa WHO ilitangaza kusimamisha  msaada wake wa kifedha huku nchi hiyo ikilaumu Shirika hilo kwa kushirikiana na kuipendelea Uchina katika harakati zake za kukabiliana na janga la COVID 19.

 Waziri wa Afya na Ustawi wa Taiwan, Chen Shih-Chung amenukuliwa akilaumu hatua ya kutoshirikishwa kwenye baraza la afya la umoja wamataifa.

Taiwan ni nchi ya visiwani katika Asia ya Mashariki upande wa kusini-mashariki wa China ina serikali yake tangu mwaka 1949 lakini Beijing inaiangalia kama sehemu ya nchi yake kufuatia historia ya nchi hizo.
Baadhi ya wanaohudhuria kikao hiki maalum ni marais wa mataifa mbalimbali ya dunia,wataalam wa afya na wageni wengine mashuhuri.

Mkuu wa shirika la Afya Duniani Tedro Adhanom anasema kuwa huu hiki ni kikao muhimu sana tangu  kuzinduliwa  1948.watu zaidi ya elfu 310,000 wamefariki kufuatia maambukizi ya Corona kote duniani huku millioni 4.7 wakiambukizwa hadi sasa.
Baadhi ya waliochangia katika mazungumzo ni Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaposa na waziri wa Afya Kenya ,Mutahi Kagwe .


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni