Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2020

dawa ya dexamethasone -corona

Picha
Virusi vya Corona na dawa ya  dexamethasone   Ni avueni kwa  wagonjwa wa COVID 19 baada ya Shirika la Afya Duniani(WHO) kukaribisha matokeo yanayoonyesha kuwa dawa ya dexamethasone inaweza kutibu na kuokoa maisha ya wagonjwa mahututi wanaougua COVID 19 au Corona. Mkurugenzi mkuu wa shirika la Afya Duniani (WHO),Dkt.Tedros Ghebreyesus anasema    utafiti huu ulifanyiwa Uingereza ambapo ,wagonjwa wa Corona waliohitaji Oksijeni na kapewa dawa hii,mmoja kati ya watano alipona.Pia waliokuwa kwenye mashine ya kusaidi kupumua walipopewa dawa ya dexamethasome,mmoja kati ya watatu alipona. Akizungumza na wanahabari mjini Gevena,Uswisi,Dkt.Ghebreyesus alisema dawa hii imekuwepo kwenye orodha ya WHO ya dawa muhimu tangu miaka ya sabini na inapatikana kwa bei nafuu katika mataifa mengi duniani. Dexamethasome ni dawa ambayo imekuwa ikitumika tangu 1960.matumishi yake yakiwa ni pamoja na kupunguza uvimbe katika maradhi tofauti mwingine ikiwemo ugonjwa wa s...

Covid-19 Ikulu Kenya

COVID 19 yabisha hodi Ikuu Kenya W afanyakazi wanne wa Ikulu ya rais nchini Kenya wamepatikana na virus vya corona hayo yemedhibitishwa na  msemaji wa Ikulu Kanze Dena. Dena amesema kuwa wafanyakazi hao waligunduliwa kuaambukizwa COVID-19 baada ya kufanyiwa uchunguzi Alhamisi wiki iliyopita. Wakanyikazi hayo wa ikulu wanaendelea kupokea matibabu katika Hospitali ya rufaa ya Chuo Kikuu cha Kenyatta. Zaidi ya hayo,Bi Dena amewahakikishia Wakenya kuwa Rais Kenyata na familia yake wake wako salama salimini na wamepatikana kutokuwa   na maambukizi ya corona. Hii ni ishara kuwa kila mtu yuko katika hatari ya kuambukizwa Corona endapo hatua zilizowekwa na Shirika la Agya Duniani na Wizara ya Afya hayatazingatiwa. Kuvaa barakoa, kuosha mikono na maji yanayotiririka na kujiepunga/kujitenga na sehemu ambapo kuwa umati ni baadhi ya masharti ya kuzingatiwa. Ikulu pia imehakikisha kuwa ili kuzuia maambukizi ya Corona kuenea , wafanyakazi wote wanaoishi nje ya Ikulu pamoja...

Rais Pierre Nkurunziza -kifo

Picha
Mke wa Rais wa Burundi aendelea kupata matibabu huku mumewe akiombolezwa Huku warundi na watu watabaka mbalimbali wakiendelea kuomboleza kifo cha aliyekuwa Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza,Mkewe angali anapokea matibabu nchini kenya kutokana na kile kinachotajwa kama maaambukizi ya virusi vya Corona. Bi Denise Nkurunziza amekuwa Nairobi kwa wiki mbili sasa,akiwa amelazwa katika hospital ya Agah Khan na matatizo ya kupumua ,ingawa hospitali hiyo imekataa kutoa taarifa ya anapoumwa Bi Nkurunziza. Kabla ya kuhamishiwa Kenya kwa matibabu,uvumi ulienea ndani na nje ya Nchi ya Burundi kuwa Mke wa Rais alikuwa kaambukizwa virusi vya Corona na alikuwa katika hali mahututi. Kuligana na hali yake ya kiafya,Bi Nkurunziza alisafirishwa nchini Kenya na Ndege ya shirika la Afya la AMREF . Mwenda zake Rais Nkurunziza anadaiwa kufariki baada ya msituko wa moyo huku uvumi uliokuwa ukienea nchini kuwa pia yeye alikuwa akiugua virusi vya Corona kukipigwa. Taarifa ya serikali ya Burundi iliyo...