Alhamisi, 18 Juni 2020

dawa ya dexamethasone -corona


Virusi vya Corona na dawa ya dexamethasone 



Ni avueni kwa  wagonjwa wa COVID 19 baada ya Shirika la Afya Duniani(WHO) kukaribisha matokeo yanayoonyesha kuwa dawa ya dexamethasone inaweza kutibu na kuokoa maisha ya wagonjwa mahututi wanaougua COVID 19 au Corona.
Koronaavaayirasii fi Qoricha: 'Dexamethasone' qoricha akkamiiti ...
Mkurugenzi mkuu wa shirika la Afya Duniani (WHO),Dkt.Tedros Ghebreyesus anasema  utafiti huu ulifanyiwa Uingereza ambapo ,wagonjwa wa Corona waliohitaji Oksijeni na kapewa dawa hii,mmoja kati ya watano alipona.Pia waliokuwa kwenye mashine ya kusaidi kupumua walipopewa dawa ya dexamethasome,mmoja kati ya watatu alipona.

Akizungumza na wanahabari mjini Gevena,Uswisi,Dkt.Ghebreyesus alisema dawa hii imekuwepo kwenye orodha ya WHO ya dawa muhimu tangu miaka ya sabini na inapatikana kwa bei nafuu katika mataifa mengi duniani.

Dexamethasome ni dawa ambayo imekuwa ikitumika tangu 1960.matumishi yake yakiwa ni pamoja na kupunguza uvimbe katika maradhi tofauti mwingine ikiwemo ugonjwa wa saratani.

Wataalamu wa afya wanasisitiza kuwa dawa hii itumiwe chini ya uangalizi mkubwa wa kimatibabu,kwani ina nguvu sana.Inatunika hasa kwa magonjwa mahututi na wanaopata matatizo ya mapavu na uvimbe katika sehemu ya mzunguko wa mapavu na moyo.

Isitoshe,dawa hii inaadhari zake:

  • Kukosa usingizi
  • Kuvuja kwa damu
  • Kutoona vizuri
  • Kuongezeka kwa uzito mwilini

Kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani(WHO) watu Zaidi ya 5,000 wamefariki kutokana na COVOD 19 kwenye bara la Afrika

Ugonjwa huu unawashabuliwa kwa hali ya juu waliona maradhi mengi tayari,kama vile kisukari,ugonjwa wa moyo na ugonjwa wa presha.


Kenya

Huku hayo yakijiri,Serikali ya kenya imetoa onyo dhidi ya matumuzi ya dexamethasone kwa
wakenya hasa kwa sababu ya madhara yake.
vya COVID 19 vimeongezeka hadi 184, ambavyo ni vya juu zaidi kuripotiwa nchini
hii leo. Vifo vya korona sasa vimefika 107 baada ya watu wawili kufariki.





Hakuna maoni:

Chapisha Maoni