Zaidi ya hayo,Bi
Dena amewahakikishia Wakenya kuwa Rais Kenyata na familia yake wake wako salama
salimini na wamepatikana kutokuwa na
maambukizi ya corona.
Hii ni ishara kuwa kila mtu yuko katika hatari ya kuambukizwa
Corona endapo hatua zilizowekwa na Shirika la Agya Duniani na Wizara ya Afya
hayatazingatiwa.
Kuvaa barakoa,
kuosha mikono na maji yanayotiririka na kujiepunga/kujitenga na sehemu ambapo
kuwa umati ni baadhi ya masharti ya kuzingatiwa.
Ikulu pia
imehakikisha kuwa ili kuzuia maambukizi ya Corona kuenea , wafanyakazi wote
wanaoishi nje ya Ikulu pamoja na wageni wamedhibitiwa huku masharti ya wizara
ya afya yakiendela kutekelezwa.
Jana waziri wa Afya ,Mutahi
kagwe alitangaza kuwa idada ya watu, walioambukizwa virusi vya corona
imeongezeka hadi 3,727.
Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, amesema pia kuna ,jumla ya 1286 waliopona katika kipindi cha saa 24.
Hata hivyo ,waziri
amewataka wakenya kuendelea kufuata mikakati iliyowekwa na serikali
ilikukabiliana na janga hili.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni