Mke wa Rais wa Burundi aendelea kupata matibabu huku mumewe akiombolezwa
Huku warundi na watu watabaka mbalimbali wakiendelea kuomboleza kifo cha aliyekuwa Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza,Mkewe angali anapokea matibabu nchini kenya kutokana na kile kinachotajwa kama maaambukizi ya virusi vya Corona.
Bi Denise Nkurunziza amekuwa Nairobi kwa wiki mbili sasa,akiwa amelazwa katika hospital ya Agah Khan na matatizo ya kupumua ,ingawa hospitali hiyo imekataa kutoa taarifa ya anapoumwa Bi Nkurunziza.
Kuligana na hali yake ya kiafya,Bi Nkurunziza alisafirishwa nchini Kenya na Ndege ya shirika la Afya la AMREF .
Mwenda zake Rais Nkurunziza anadaiwa kufariki baada ya msituko wa moyo huku uvumi uliokuwa ukienea nchini kuwa pia yeye alikuwa akiugua virusi vya Corona kukipigwa.
Taarifa ya serikali ya Burundi iliyotolewa kwa umma inadhibitisha kuwa amefariki kutokana na mshtuko wa moyo.
Rais Nkurunziza ametawala Burundi kwa miongo mitatu yaani miaka kumi na tano na amefariki siku chache baada ya uchanguzi wa nchi hiyo,ambapo Generali Evariste Ndayisimiye alitangazwa mshindi wa uchaguzi huyo.
Nkurunziza alitalajiwa kumkabidhi mamlaka Rais huyo mteuliwa mwezi wa nane ,mwaka huu.
Serikali ya Burundi imetanga maobolezi ya kitaifa huku bendera ya nchi hiyo ikipeperushwa nusu mlingoti.
Mola awape afueni wenye majonzi.
Presha au shinikisho la damu
Mshtuko wa moyo unatokea wakati damu inapiga
kwa wingi na mishipa ikiwa miyembamba. Watu wengi hufariki ghafla baadha ya
mstuko wa moyo. Wataalam wa afya wanasema kuwa hali hii inauwa watu wengi bila
kuonyesha dalili huku wakisisitisha umuhimu wa kupimwa mara kwa mara.
Kipimo cha shinikizo la damu kawaida ni
100–140 mmHg kipimo cha juu na 60–90 mmHg kikiwa kipimo cha chini. Shinikizo la
juu la damu hutokea kipimo kikiwa zaidi ya 140/90 mmHg kwa muda mrefu.
Ugonjwa huu isipogunduliwa mapewa unaweza
kusababisha madhara ya kiafya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni