Viongozi na wajumbe kutoka takriban nchi 200 wanakongamana kwenye kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya hali ya anga,ambalo limengoa nanga huko Glasgow,Scotland,leo Katika mkutano huu wa COP26, maswala kadha yatajadhiriwa hususan jinsi ya kupunguza utoaji gesi ya carbon kufikia mwaka 2030 na kunusuru dunia kutoa kwa adhari za mabadiliko ya hali ya anga.
Kongamano hili litafanyika kwa majuma mawili,huku fursa ya kwanza ikitolewa kwa Shirika la utabiri wa hali ya anga duniani ili kutoa ripoti kuhusu hali ya anga ilivyo kufikia sasa.Lengo likiwa kutathmini viwango vya joto duniani kufikia mwaka huu na miaka ya awali. Zaidi ya hayo, ripoti imeandaliwa na itatolewa na wanasayansi wa hali ya anga.
Hali ya anga imebadilika kwa kasi huku shughuli za wanadamu zikitolewa kama chanzo kuu cha mabadiliko hayo. Viwango vya juu zaidi vya joto, mafuriko na moto misituni inazidi kuongezeka,jambo ambalo linatia hofu.
Mkutano huu unafanyika baada ya mwingine kama huu, uliofanyika jijini Paris,Ufaransa ambapo mataifa yaliafikia kwa kauli moja kuweka mikakati ili kukabili tatizo hili.Hivyo basi ,wajumbe watatoa ripoti ni vipi mataifa yao yamefanya ili kupunguza viwango vya joto,tangu kongamano la Umoja wa Mataifa la 2015,lijulikanalo kama asimio la Paris.
Rais wa Jamhuri ya Kenya,Uhuru Kenyatta anaongoza
ujumbe kutoka Kenya na anatarajiwa kutoa ripoti kuhusu hatua ambazo Kenya
imechukua kukabiliana na mabadiliko ya hali ya anga.
Isitoshe,Kenya imekuwa kwenye mstari wa mbele kutoa mikakati ili kukabiliana na mabadiliko ya hewa .
Taifa la Kenya lilipiga hatua na likawa la kwanza Afrika kupitisha sheria kuhusu mabadiliko ya hali ya anga mwaka 2016.Ilikubaliana kwamba asilimia 90 ya umeme unaotumika usiwe na madhara yoyote na inalenga kuafikia asilimia 100 mwaka 2030.Tayari Kenya inapata umeme kutoka kwa maji,upepo,jua na mvuke.Wakenya wameanza kukumbatia na kuutumia umeme huu kwani hauna madhara yeyote.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni