Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2022

TB day

Siku ya Kifua Kikuu Duniani Siku ya Kifua Kikuu (TB) Duniani huamasishwa Machi 24kila mwaka.lengo likiwa kufahamisha umma idadi ya maabukizi,vifo, juhudi za kukomesha janga la TB na binu mpya zinazobuniwa ili kukabiliana na makali ya ugonjwa wa TB. Mnamo Tarehe mwaka wa 1882 Dk Robert Koch alitangaza kwamba amegundua bakteria inayosababisha TB, ambayo ilitoa fursa ya kutambua na kuponya ugonjwa huu. TB inasalia kuwa moja ya magonjwa hatari zaidi ya kuambukiza ulimwenguni. Kila siku, zaidi ya watu 4100 hupoteza maisha kwa TB na karibu watu 28,000 wanaugua ugonjwa huu unaozuilika na pia kutibika. Juhudi za kimataifa za kukabiliana na TB zimeokoa maisha ya takriban milioni 66 tangu mwaka wa 2000. Hata hivyo, janga la COVID-19 limerudisha nyuma maendeleo ya miaka mingi iliyopatikana katika vita vya kukomesha TB. Kwa mara ya kwanza katika zaidi ya muongo mmoja, vifo vya TB viliongezeka mwaka 2020. Kauli mbiu ya Siku ya Kifua Kikuu Duniani mwaka huu-2022, ni ‘Wekeza Kukomesha Kifua K...