Ijumaa, 24 Agosti 2012

Martin Shikuku aaga dunia-Saratani


Ugonjwa wa saratani umetupokonya mwanasiasa mkongwe mzee Martin Shikuku.

Mzee Shikuku aliaga dunia katika hospitali ya Texas ambayo ni kituo cha  kipekee cha matibabu cha ugonjwa wa saratani.

Shikuku alikuwa akipata matibabu katika kituo hicho kwa miezi kadha.
Shujaa Shikuku alikuwa tayari alijizika akiwa hai kwa kujichimbia kaburi na kukamilisha kushughuli zingine ambazo zinaambatana na maziko.

Mbunge huyo wa zamani wa Butere alikuwa mstari wa mbele katika harakati ya kutaka mfumo wa vyama vingi na pia mtetezi wa haki za wanyonge.

Alijipata matatani na Uongozi wa rais mstaafu Daniel Moi alipoungana na viongozi wengine kuaada mkutano wa hadhara katika uwanja wa kamukunji, kutetea mvumo wa vyama vingi.

Alifungwa lakini hakukoma kumkosoa viongozi wafisadi na waliojipenda na kusahau kuwakilisha wananchi inavyostahili.

Kwake hayati Shikuku,siasa ilikuwa ni witu wala si kujinufaisha.Miezi miwili iliyopita Waziri Mkuu Raila Odinga alimtembelea hopitalini na kuahidi kuwa serikali ingemlipia gharama ya hospitali. 

Hakika Shikuku ulikuwa mzalendo.

Mungu alilaze roho ya hayati mahali pema peponi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni