Jumanne, 26 Februari 2013

Anyang Nyong'o vita dhidi ya saratani

 Saratani

Vita dhidi ya ugonjwa wa saratani umeimarishwa baada ya waziri wa huduma za matibabu ya umma Nyang nyong'o  kutangaza kuwa shirika mmoja la Uingereza limetoa fedha zaidi ya shillingi 517 billion kugharamia ujenzi wa kituo cha saratani nchini Kenya.

Hii ni afueni kwa wakenya hususan wanaougua saratani watapata matibabu bila kusubiri kwa miezi kama hali ilivyo kwa sasa.

Hospitali kuu ya Kenyatta inahudhumia wakenya kutoka sehemu zote za nchi, jambo ambalo linafanya wengi kusubiri kwa miezi tano na zaidi kabla ya kuhudumiwa.

Kulingana na takwimu za afya, wakenya 18,000 hufariki kutokana na maradhi ya saratani kila mwaka.Pia vifaa vinanavyotumiwa kutibu na kuutafiti ugonjwa huu ni duni na vya kiwango cha chini ikilinganishwa na mataifa yalitiyostawi.

Ili kukabiliana na saratani kwa undani, Rais Mwai kibaki mwaka jana alipitisha sheria ya saratani"cancer prevetion Bill 2012 ilikuhakikisha kuwa wanaougua saratani wanapata huduma bora ya afya.




Samuel kivuitu aiaga dunia



Aliyekuwa mwenyekiti  wa iliyokuwa tume ya uchaguzi   ECK Samuel Kivuitu ameaga dunia.

Kivuiti mwenye umri wa miaka 74 amekuwa akiigua saratani ya  koo.
Kwa mujibu wa msemaji wa  familia yake,Mzee Kivuitu amefariki dunia katika hospitali ya MP Shah mjini Nairobi alipokuwa akipata matibabu ya maradhi ya kansa. Taarifa zaidi zinasema, Kivuitu amekuwa akiugua  kwa muda wa miaka miwili sasa.Amekuwa akipokea matibabu ndani na nje ya nchi. Matokeo ya uchaguzi wa rais nchini Kenya mwaka 2007 yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ya Kenya wakati huo ECK chini ya uwenyekiti wa Samuel Kivuitu yalipelekea kutokea machafuko makubwa kuwahi kushuhudiwa katika historia ya Kenya ambapo watu 1,133 waliuawa na wengine laki sita na nusu kubaki bila makazi.
Kifo cha Kivuitu kimetokea wiki moja kabla ya uchanguzi mkuu unaotarajiwa  kufanyika mapema mwezi ujao.