Aliyekuwa mwenyekiti wa iliyokuwa tume ya uchaguzi
ECK Samuel Kivuitu ameaga dunia.
Kivuiti
mwenye umri wa miaka 74 amekuwa akiigua saratani ya koo.
Kwa mujibu wa msemaji wa familia yake,Mzee Kivuitu amefariki dunia
katika hospitali ya MP Shah mjini Nairobi alipokuwa akipata matibabu ya maradhi
ya kansa. Taarifa zaidi zinasema, Kivuitu amekuwa akiugua kwa muda wa miaka miwili sasa.Amekuwa akipokea matibabu ndani na nje ya nchi. Matokeo
ya uchaguzi wa rais nchini Kenya mwaka 2007 yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi
ya Kenya wakati huo ECK chini ya uwenyekiti wa Samuel Kivuitu yalipelekea
kutokea machafuko makubwa kuwahi kushuhudiwa katika historia ya Kenya ambapo
watu 1,133 waliuawa na wengine laki sita na nusu kubaki bila makazi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni