Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2013

world malaria day

Picha
 siku ya malaria duniani Huku dunia ikiadhimisha siku ya Malaria  hii leo, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon ametoa ujumbe na kusema kuwa bado ugonjwa huo ni tishio  kwa nchi maskini hususan barani Afrika, ambako mamilioni ya watu wanashindwa kujikinga dhidi ya Malaria.  Isitoshe,Bwana Ban amesema barani Afrika kila dakika mtoto mmoja anafariki dunia kutokana na ugonjwa huo na kwamba mifumo dhaifu ya ufuatiliaji inakwamisha uwezo wa serikali na shirika la afya duniani, WHO kupata taarifa za kina kuhusu maeneo mapya yenye ugonjwa huo na mabadiliko ya mwenendo wa ugonjwa huo. Amesema usugu wa vijidudu vya Malaria dhidi ya dawa za kunywa na hata katika vyandarua vyenye viuatilifu, unafanya hali kuwa mbaya zaidi kuweza kutokomeza ugonjwa huo na hivyo kutishia uhai na maendeleo.   Kauli mbiu inayoongoza Maadhimisho ya Siku ya Malaria Duniani kwa Mwaka 2013; Wekeza kwa siku za baadaye. Shinda Malaria. Bwana Ban amesema  ameisihi...

Thatcher 08/ 04/ 2013

Picha
Thatcher  aaga dunia London Uingereza - Waziri mkuu wa zamani wa Uingereza Margaret Thatcher ambaye alikuwa akijulikana kama "Iron Lady" kwa ukakamavu wake ambaye amezifanyia marekebisho siasa za kizazi cha Uingereza amefariki dunia baada ya kupigwa na kiharusi leo akiwa na umri wa miaka 87. Mengi zaidi na Mohammed Dahman. Malkia Elizabeth wa Pili wa Uingereza na Waziri Mkuu David Cameron wameongoza katika salamu za rambi rambi kwa waziri mkuu huyo wa kwanza mwanamke nchini Uingereza, muumini mashuhuri kabisa wa sera za mrengo wa kulia na mtu muhimu wakati wa Vita Baridi. Msemaji wa familia ya Thatcher amekaririwa akisema "kwa masikitiko makubwa Mark na Carol Thatcher (watoto wa marehemu) wanatangaza kwamba mama yao Bi. Thatcher amefariki kwa utulivu baada ya kupigwa na kiharusi leo asubuhi." Waziri Mkuu huyo wa zamani ambaye aliiongoza Uingereza kuanzia mwaka 1979 hadi mwaka 1990 alikuwa akikabiliwa na maradhi ya kupoteza kumbukumbu na mara c...