Huku Vifo vya wanawake wajawazito wakati wa kujifungua vikisalia kuwa tishio, Kenya inakabiliwa na changamoto ya ugonjwa wa fistula, ambao hutokea mama anapojifungua baada ya uchungu wa muda mrefu na kuacha tundu katika sehemu ya haja ndogo hadi haja kubwa. Kulingana na Shirika la Umoja la idadi ya watu duniani UNFPA, kati ya visa 3000 vya Fistula ambavyo vinatokea kila mwaka nchini Kenya, ni asilimia 7 tu ya wanawake wanapata huduma za matibabu. wanawake wazungumzia unyanyapaa waliyokumbana nayo baada ya kuugua Fistula. Katika hospitali kuu ya Kenyatta wengi wamesahauliwa na pia kutengwa na jamii. Lakini sasa wana sababu ya kutabasamu baada ya kupata matibabu ya upasuaji. Mama Monica Mwangi kwa sasa anasema amepona na amatarajia kurundi nyumba bila aibu. Hospitali ya Kenyatta imeanzisha kampeini ya kupambana na ugonjwa huu kila mwaka matibabu ya bure yakitolewa kwa wakenya na wagonjwa wengine nchini.
Machapisho
Inaonyesha machapisho kuanzia Julai, 2015
cancer conference Nairobi
- Pata kiungo
- X
- Barua pepe
- Programu Nyingine
Saratani Kongamano kuhusu ugonjwa wa saratani la kamilika nchini Kenya, huku idadi ya waathiriwa ikiongezeka na upungufu wa vituo vya afya vikiwa adimu. Tatizo pia la gharama linawazuia wengi kutafuta usaidizi wa kimatibabu. Akizungumza Hivi majuzi katika kikao kilichojadili maradhi hayo, kwenye kongamano la tisa la Kukomesha Saratani ya Mlango wa Kizazi, Matiti na Tezi Kibofu, Bi Kenyatta pia alisema kuwa idadi kubwa ya watu wanaogopa kutafuta matibabu kwa sababu ya unyanyapaa uliopo katika jamii na ukosefu wa rasilmali za kutosha kukabiliana nao. Rais Uhuru Kenyatta ameahidi kuwahimiza marais wenzake kote ulimwenguni kutenga pesa za kutosha kukabiliana na saratani. Rais aliahidi hayo katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa wake wa marais na wajumbe wanaohudhuria kongamano hilo la siku tatu . Rais alitoa ahadi hiyo baada ya kutuzwa na kutambuliwa na wake hao wa marais kama “Balozi wa Nia Njema Afrika kwa Afya ya Wanawake na Watoto” hapo Jumata...