Alhamisi, 30 Julai 2015

cancer conference Nairobi

Saratani
Kongamano kuhusu ugonjwa wa saratani la kamilika nchini Kenya,  huku idadi ya waathiriwa ikiongezeka na upungufu wa vituo vya afya vikiwa adimu.

 Tatizo pia la gharama linawazuia wengi kutafuta usaidizi wa kimatibabu.

Image result for margaret kenyatta cancer conference kenyaAkizungumza  Hivi majuzi katika  kikao kilichojadili maradhi hayo, kwenye kongamano la tisa la Kukomesha Saratani ya Mlango wa Kizazi, Matiti na Tezi Kibofu, Bi Kenyatta pia alisema kuwa idadi kubwa ya watu wanaogopa kutafuta matibabu kwa sababu ya unyanyapaa uliopo katika jamii na ukosefu wa rasilmali za kutosha kukabiliana nao.

Rais Uhuru Kenyatta ameahidi kuwahimiza marais wenzake kote ulimwenguni kutenga pesa za kutosha kukabiliana na saratani.

Rais aliahidi hayo katika hafla ya chakula cha jioni iliyoandaliwa wake wa marais na wajumbe wanaohudhuria kongamano hilo la siku tatu .

Rais alitoa ahadi hiyo baada ya kutuzwa na kutambuliwa na wake hao wa marais kama “Balozi wa Nia Njema Afrika kwa Afya ya Wanawake na Watoto” hapo Jumatatu. Kutambuliwa huko kunamhitaji aendelee kutetea kuimarishwa kwa afya na hasa masuala ya saratani miongoni mwa marais wenzake.

Zaidi ya hayo, rais alisema kuwa saratani imesababisha uchungu mwingi kwa familia nyingi kwani mbali na kuathiri afya yao.

Image result for margaret kenyatta cancer conference kenya
Bi Kenyatta ambaye ndiye mwenyekiti mpya wa muungano huo wa wake wa marais wanaokabiliana na saratani, aliahidi kushirikiana na wizara ya afya, viongozi wa kidini na kitamaduni na mashirika ya kijamii pamoja na vyombo vya habari kutetea wafanyakazi na pesa za kutosha kukabiliana na saratani.

Alielezea matumaini kuwa teknolojia inayoendelea kuongezeka itasaidia katika uchunguzi na matibabu ya maradhi hayo ya saratani.Pia alipongeza serikali kwa kuanzia

 Taasisi ya Kitaifa ya Saratani kuongoza vita dhidi ya saratani nchini, akisema kuwa taasisi hiyo itasaidia kutoa data ambayo ni muhimu katika juhudi za kukabiliana na maradhi hayo.“Nchini Kenya, hali inatia hofu, kuna visa zaidi 3,000 vya saratani ya mlango wa kizazi vinavyogunduliwa kila mwaka ambapo nusu huishia kwa vifo kwa sababu ya kugunduliwa kuchelewa,” alisema Rais Kenyatta mapema Jumatatu alipofungua rasmi kongamano hilo katika ukumbi wa mikutano wa KICC.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni