Alhamisi, 30 Julai 2015
Huku Vifo vya wanawake wajawazito wakati wa kujifungua vikisalia kuwa tishio, Kenya inakabiliwa na changamoto ya ugonjwa wa fistula, ambao hutokea mama anapojifungua baada ya uchungu wa muda mrefu na kuacha tundu katika sehemu ya haja ndogo hadi haja kubwa.
Kulingana na Shirika la Umoja la idadi ya watu duniani UNFPA, kati ya visa 3000 vya Fistula ambavyo vinatokea kila mwaka nchini Kenya, ni asilimia 7 tu ya wanawake wanapata huduma za matibabu. wanawake wazungumzia unyanyapaa waliyokumbana nayo baada ya kuugua Fistula.
Katika hospitali kuu ya Kenyatta wengi wamesahauliwa na pia kutengwa na jamii.
Lakini sasa wana sababu ya kutabasamu baada ya kupata matibabu ya upasuaji.
Mama Monica Mwangi kwa sasa anasema amepona na amatarajia kurundi nyumba bila aibu.
Hospitali ya Kenyatta imeanzisha kampeini ya kupambana na ugonjwa huu kila mwaka matibabu ya bure yakitolewa kwa wakenya na wagonjwa wengine nchini.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni