Jumanne, 9 Februari 2016

Stop FGM

FGM HOTUBA 


Huku siku ya kimataifa kukabiliana na ukeketaji ikiadhimishwa, takwimu zinaonyesha idadi ya watu waliokeketwa imeongezeka kote duniani. Kulingana na shirika la watoto duniani(UNICEF) inakisiwa wanawake milioni 200 walikeketwa mwaka uliopita (2015) duniani.

 Ethiopia,Indonesia na Misri zinatajwa kama baadhi ya nchi ambazo zimechangia kwa wingi kuendeleza kitendo hiki cha kudunisha mwanamke. 

Kuna ripoti pia kuwa Kenya ,mashirika ya jamii ambayo yanastahili kuwa mstari wa mbele kupambana na hali hii , yameshindwa kukabiliana na visa vya ukeketaji katika maeneo mengi ambako ukeketaji umekidhiri.

 Jambo la kutamausha ni kuwa kanisa pia limehuzishwa na shughuli hii,kwa kuwasaidia wakeketwa kupata ukeketaji hospitalini,ambao unatajwa kama nafuu kuliko kupitia hali ya kitamadhuni ambayo inaabatanishwa na hatri nyingi. 

Kulingana na sheria za nchini Kenya,ukeketaji ni hatia na yeyote atakaye patikana akitekeleza shughuli hizo atakuchuliwa hatua za kisheria. 

Huku kampeini dhidi ya ukeketaji sikiendelezwa nchini Kenya ,sehemu ambazo zimeadhiriwa zaidi,wengi hawajui kusoma wala kuandika ,hii ikichangia kuongezeka kwa tisho hili.

 Katika sehemu za kajiado wasichana walivunja damu hadi wakafariki huku wakikeketwa ,huku baadhi ya ngariba wakionyesha ukaidi na kuendelea kukeketa wasichana kwa malengo ya kuhifadhi mila na tamaduni za wamaasai.

 Ngarima na akina mama Kajiado wakati mmoja wali fanya maadamana kupinga sheria ya kukabiliana na ukeketaji. Walisema muacha mila ni mtumwa na ni sharti waendeleze shughuli ambayo inaenziwa na jamii yao. 

Hivyo basi ni jukumu la jamii na serikali kuungana pamoja kuangamiza ukeketaji kwa manufaa ya mtoto wa kike na wanawake kwa jumla.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni