Jumanne, 9 Februari 2016

Ukeketaji(FGM)

Janet Kathambi angali mwenye machungu na kilio moyoni anapokumbuka jinsi kikundi cha wanawake kilivyomvamia alipokuwa akiteka maji kisimani,katika jimbo la Meru,nchini Kenya.

 Ilikuwa siku ya jumamoshi alipokuwa katika shunguli zake kuteka maji,aliposikia kelele ilioandamana na nyimbo za kejeli kwa wanawake ambayo hawaja keketwa. 

Alipigwa na butwaa kwani walimtishia mara kwa mara kuwa wangemwadhibu endapo hangekubali kukeketwa. Lahaula ,kufuba na kufungua macho walimuinua juu na kumubeba huku wakimfanyia dhihaka.

 Walimpeleka moja kwa moja hadi kwa ngarimba aliyemshughulikia na baadaye wakampeleka kwake . Jambo hili halikumghadhabisha mumewe kwani alitaka pia akeketwe ili amuondolee aibu na dharau kutoka kwa wanaume wa rika lake.

 Hii ni baadhi ya matatizo au aibu wanasozipitia wanawake ambayo hawaja tahirishwa katika baadhi ya sehemu nchini Kenya. Hata baada ya serikali kuelimisha watu hatari na madhara yanayoabatana na ukeketaji,tabia hii potovu inaendelea . 

Takwimu zinaonyesha kuwa wanawake million 9.3 wamepitia uchungu na tishio la ukeketaji. Huku maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kukataa ukeketaji kote duniani ikiadhimishwa Jomamoshi iliyopita , hali ingali mbaya na hatua madhubuti zahitajika kukomeza tatizo hili. 

Kauli mbiu ya mwaka huu ikiwa .Pamoja tuangamize ukeketaji sasa, ni jukumu letu kushirikiana na kueneza habari kuwa ni hatari kuendeleza mbinu au dhana iliyopitwa na wakati kwa kuzingizia mila na tamaduni .

 Isitoshe ni jambo muhimi kwa mashirika husika na wadau wengine kutilia maanani swala hili ilikuhakikisha idadi ya wanaokeketwa haiongezeki kila kuchao. 

Afya ya uzazi huadhiria zaidi na ukeketaji ,kwani mwanamke hupata shida anapojifungua na pia matatizo ya fistula yamewapata akina mama . Mila hii pia humfanya motto wakike kuwa hatarini yakuozwa mapema.Punde tu anapokeketwa kuna mume tayari kumuoa. 

Hii imechangia pia ongezeko la watoto wengi kutohudhuria masomo,huku wengine wakitoroka nyumbani kutafuta usaidizi kwa serikali. Mwenyekiti wa halmashauri inayokabiliana na kutoa elimu kuhusu madhara ya ukeketaji,Lina Jebii Kilimo amesema kuna haja ya kuwaerimisha wanafunzi shuleni na vyuoni madhara ya tohara. 

Ukeketaji umeenea sana sehemu za Kuria,Kisii,maeneo ya Kajiado,Samburu,Meru na pia Kaskasini Mashariki. "Vita dhidi ya ukeketaji vimeimarishwa nchini Kenya, huku elimu na mijadala ikitolewa ilikupinga dhana inayohuzishwa na ukeketaji "asema Kilimo Serikali ilibuni harimashauri ya kitaifa ,kwa minajili ya kukomesha dhana hii potofu.

Kulingana na wanachama wa harimashauri inayoshughulikia na kutafuta mbinu mwafaka za kuangamiza ukeketaji, mikakati imeweka kuhakikisha kuwa mafunzo kuhusu madhara ya tohara kwa wasichana na wanawake majimboni. 

Kufuatia hatua kali za kisheria watu wengi wangali wanakeketa hospitalini kwa siri. Wengi wanaamini kuwa wanamke asiyekatwa ni kero kwa jamii. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni