Masaibu ya wagonjwa katika
hospitali ya Mama Lucy Kibaki
Mama Lucy Kibaki hospitali
iliyoko Embakasi imegonga vyombo vya habari kwa sababu za kuhuzunisha.
Visa vya wagonjwa kutohudumiwa
ipasavyo na madai ya ukosefu wa vifaa vya matibabu vinahusunisha.
Kisa cha kustajabisha ni kuwa
madaktari walimwacha mama mja mzito bila kuhudumiwa kwa muda hadi wanawe mapacha
kufia kwenye kizazi.
Imedaiwa kuwa mtoto aliyekuwa na
majeraha ya ajari aliruhusiwa kwenda nyumbani hata kabla ya uchunguzi wa kina
kuhakikisha kuwa maisha yake hayakuwa hatarini
Mamake mtoto anasema mwanawe
aliaga dunia siku oja baada ya kwenda nyumbani.
Baadaye daktari katika hospitali
hiyo wakamfahamisha kuwa alivuja damu kwa ubongo,kwani alikuwa na majeraha
jichoni.
Hayo ni baadhi ya masaibu
yanayowakuba wagonjwa kwenye Hospitali ambayo ni ya pili kwa ukubwa jijini
Nairobi na ya tatu nchini.
Madhumuni ya kuanzisha hospitali
hii ilikuwa kupunguza idadi kubwa ya wagonjwa katika hospitali kuu ya Kenyatta
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni