Jumanne, 9 Februari 2016

Madaktari walaghai India



Saratani 

Kuna madai kuwa baadhi ya madaktari nchini Kenya wanapokea hongo ilikuwapa barua wagonjwa wa saratani kutafuta matitabu nchini India.

 Hii imepelekea waziri wa afya nchini kutangaza kuwa uchunguzi umeanzishwa kwa nia ya kubaini iwapo madai hayo ni ya kweli . 

Kulingana na mtaalam wa saratani Daktari David makumi,kuna baadhi ya madaktari wanaochukua ripoti za madaktari nchini Kenya na baadaye kuwapingia simu na kuwahidi kitita cha pesa endapo wangeshirikiana kutuma wagonjwa. 

Imekuwa kama biashara huku kukiwa na madaktari ambao hakika na ujuzi wa kutibu saratani nchini. Hapo awali,wakenya walisema lengo muhimu la kutafuta matibabu India ni kwa sababu za kifedha.

Kenya matibabu ya saratani ni ghali ikilinganishwa na Nchini India. Pia hakuna msongamano kama ilivyo Kenya. 

Wagonjwa pia wanasema mashine za kutibu saratani India ni za Hali ya juu,kitekinologia zikilinganisha na Kenya. 

Baadhi ya wagonjwa hulazimika kusubiri kwa muda mrefu kupokea matibabu,hususan katika hospitali za kitaifa. 

Wasio na uwezo wakifedha pia hupata matatizo na kuamua kubaki nyumbani wakisubiri hati yao ya mauti. Ingawa bina ya kitaifa ya afya inachangia malipo ya matibabu,kuna wengi ambao hawajasajiliwa kwani hawana pesa ya kulipa kwa shirika hilo kila mwezi.

 Hii pia ni changamoto ambayo serikali inapashwa kushughulikia. Kutafuta mbinu mwafaka kuona kila mmoja anapaka matibabu anapoungua bila kutengwa au kupuuzwa na maana hawana uwezo wakuchangia.

 Hivi majuzi visa vya wagonjwa wa saratani kuzuiliwa hospitalini India zimeripotiwa na zinaongezeka kila kuchao. Endapo madai haya yatadhibitishwa kuwa kweli basi huu ni ulaghai wa hali ya juu,na haku na budi kuwachukulia hatua za kisheria wahusika. 

Ni jambo la aibu kutumia hali ya mgonjwa kujinufaisha na kunufaisha mataifa ya nje . Uzalendo umefifia au umekufa ikiwa hii leo ,mgonjwa ambaye anaweza kutibiwa nchini Kenya atafahamishwa kuw hali yake inaweza tu kutibiwa nchini India au nchini ingineyo. 

Hakika madaktari kama hayo wanastahili wasiruhusiwe kufanya kazi yao kokote pale kwani ,ikiwa ni kweli, ni walafi,walaghai na pia wafisadi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni