Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Machi, 2016

Josephine Nyambura aaga duniani cancer

Picha
Maoni Ugonjwa wa saratani waendelea kukusababisha maafa. Idadi ya wanaofariki kufuatia maradhi hayo yanaongezaka kila kuchao.  Ni hali ya kuhuzunisha kuona kuwa Wasio na uwezo wa kugharamia matibabu ndio wanaoadhirika zaidi.  Ni jukumu la serikali kutafuta mikakati ku ona kwamba watu wote wanapata matibabu bila vikwazo vyovyote. Huduma ya bima ya kitaifa inapashwa pia kusaidia wenye uwezo wa kulipa malipo ya kila mwezi na pia wasioweza.  Malkia Josephine Nyambura aaga duniani . Mtoto wa miaka nne ambaye hivi majuzi alikosa kupata matibabu ya ugonjwa wa saratani kufuatia matatizo ya kifedha yaliyoikuba familia yake aaga duniani.  Malkia Josephine Nyambura alinyimwa matibabu na madaktari nchini India na kwa kuwa hali yake ilikuwa hatarini wawazi   wake wakamrejesha nchini Kenya katika hospitali kuu ya Kenyatta ambayo pia Imekuwa na upungufu wa mashine za saratani.  Hali yake ilizorota baadaye huku mwili wake kufula. Saratani ya damu aliy...

ZIka Chanjo -Vaccine

Picha
Huku ugonjwa wa Zika ukiendelea   kuenea kwa kasi,kampuni ya   dawa ya ufaransa -Sanofi Pasteur iko katika harakati   na shughuli za kukomesha virusi vya Zika. Kwa sasa kuna mikakati ya kufanya utafiti wa chanjo kwa binadamu ili kuepuka adhari za ugonjwa wa Zika. Kulingana na Nicholas Jackson, ambaye anaongoza kundi la watafiti ,shabaha yao ni kuhakikisha wamepata tiba ya virusi vya Zika haraka iwezekanavyo. Ingawa utafiti wa chanjo huchukua muda- mrefu,miaka ishirini na zaidi- kundi hili lina matumaini   kuwa watafanya wawezalo kuhakikisha tiba imepatikana kwa muda mfupi. Zaidi ya hayo,Mtafiti Jackson,ananukuliwa akisema ,kampuni ya Sanofi Pasteur inaweza kutumia ufundi,vifaa na uzoefu vilivyotumia katika utafiti na utengenezaji wa chanjo ya virusi ya Dengue miaka kadha iliyopita,katika shughuli   za utafiti na chanjo ya virusi vya Zika. Kampuni hiyo ina umaarufu na pia   inaongoza duniani katika utafiti wa chanjoya virusi vya Homa ya Majano.C...