Jumanne, 8 Machi 2016

Josephine Nyambura aaga duniani cancer


Maoni
Ugonjwa wa saratani waendelea kukusababisha maafa.

Idadi ya wanaofariki kufuatia maradhi hayo yanaongezaka kila kuchao. 
Ni hali ya kuhuzunisha kuona kuwa Wasio na uwezo wa kugharamia matibabu ndio wanaoadhirika zaidi. 

Ni jukumu la serikali kutafuta mikakati ku
ona kwamba watu wote wanapata matibabu bila vikwazo vyovyote.
Huduma ya bima ya kitaifa inapashwa pia kusaidia wenye uwezo wa kulipa malipo ya kila mwezi na pia wasioweza. 



Malkia Josephine Nyambura aaga duniani.

Mtoto wa miaka nne ambaye hivi majuzi alikosa kupata matibabu ya ugonjwa wa saratani kufuatia matatizo ya kifedha yaliyoikuba familia yake aaga duniani. 

Malkia Josephine Nyambura alinyimwa matibabu na madaktari nchini India na kwa kuwa hali yake ilikuwa hatarini wawazi   wake wakamrejesha nchini Kenya katika hospitali kuu ya Kenyatta ambayo pia Imekuwa na upungufu wa mashine za saratani. 
Hali yake ilizorota baadaye huku mwili wake kufula.

Saratani ya damu aliyokuwa akiugua mtoto inaweza tibia kwa asilimia 70 hasa nchini India , kutoka na vifaa vya kiteknologia vinavyotimiwa,  ikilinganishwa na hapa nchini Kenya. 
Gharama ya matibabu ya saratani ni ghali mno na kwa familia hii kwa upendo wa mwanao waliuza mali yao yote ili mtoto wao apate matibabu , lakini hata baada ya hayo yote.

Gharama iliendelea kuwa kikwazo hadi wakalazimika kukatiza matibabu huko India. 
Kabla ya kufarikiyule,Malkia b alimhakikishia babake kuwa hatafarki kama njia moja ya kuwaongezea matumaini wakazi wake walioonekana kuhuzuniswa na hali yake. 

Jambo la kutamausha ni kuwa hata baada ya habari za mtoto Malkia Nyambura kuangaziwa na vyombo vya habari hatua za kutafuta pesa za matibabu hazikufua dafu.
Imekuwa ni safarini yenye Milima na mabonde kwa mtoto na wazaziwe .

Mola awape amani familia yake Malkia na wengine wanapitia hali hii ngumu.

Malkia lala salama. 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni