Ijumaa, 4 Machi 2016

ZIka Chanjo -Vaccine


Huku ugonjwa wa Zika ukiendelea  kuenea kwa kasi,kampuni ya  dawa ya ufaransa -Sanofi Pasteur iko katika harakati  na shughuli za kukomesha virusi vya Zika.
Kwa sasa kuna mikakati ya kufanya utafiti wa chanjo kwa binadamu ili kuepuka adhari za ugonjwa wa Zika.
Image result for zika vaccineKulingana na Nicholas Jackson, ambaye anaongoza kundi la watafiti ,shabaha yao ni kuhakikisha wamepata tiba ya virusi vya Zika haraka iwezekanavyo.
Ingawa utafiti wa chanjo huchukua muda- mrefu,miaka ishirini na zaidi- kundi hili lina matumaini  kuwa watafanya wawezalo kuhakikisha tiba imepatikana kwa muda mfupi.

Zaidi ya hayo,Mtafiti Jackson,ananukuliwa akisema ,kampuni ya Sanofi Pasteur inaweza kutumia ufundi,vifaa na uzoefu vilivyotumia katika utafiti na utengenezaji wa chanjo ya virusi ya Dengue miaka kadha iliyopita,katika shughuli  za utafiti na chanjo ya virusi vya Zika.

Kampuni hiyo ina umaarufu na pia  inaongoza duniani katika utafiti wa chanjoya virusi vya Homa ya Majano.Chanjo yake ilipata kibali cha kutumiwa katika nchi za Brazil,Mexico na ufilipino.
Sanofi  imechukua hatua ambayo  tayari kampuni zingine za dawa kama vile;  Bharat Biotech ya India,  Inovio naTaasisi ya afya ya kitaifa ya Marekani(  U.S. National Institutes of Health) -kampuni za marekani  zimezindua utafiti wa tiba ya Zika.
 Jaribioya chanjo hiyo kwa binadamu henda ikawa mwaka ujao,ikiwa mikakati iliowekwa itafikiwa bila shida yeyote.
Haijabainika hakika ikiwa virusi vya Zika vinasababisha motto kzaliwa na kichwa kidogo ,lakini kuna uhusiana wa kuabatanisha hali hiyo na virusi hivyo.
Shirika la Afya Duniani(WHO) linakisia kuna idadi ya 15 kampuni na wasomi ambao kwa sasa wanatafiti tiba ya Zika.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni