Jumatano, 27 Aprili 2016

Malaria Kenya


Idadi ya wagonjwa wa  malaria yapungua Kenya

Ugonjwa wa malaria umekuwa ni tisho katika maeneo yenye joto Afrika hususan nchini Kenya.
Image result for malaria mosquito kenyaJambo la kutia moyo ni kwamba  iadadi ya watu wanaougua ugonjwa huu umepungua marudufu kwa miaka sita iliyopita.

Kulingana na tafiti za wizara ya Afya hali hii inatokana na ongezeko la utumiaji viandarua na pia kupata matibabu mapema.Msemaji wa wizara ya afya Elisha Omondi anasema hatua za serikali za kuukabili ugonjwa wa malaria zimezaa matunda.
Hata hivyo sehemu kama vile  jimbo la Siaya linaongoza kwa maambukizi hayo,lakini pia katika kipindi cha mwaka mmoja angalau asilimia 50 ya visa vimekabiliwa.
Majimbo ya Pwani pia yameadhirika lakini hali sio mbaya kama siku za nyuma.
Takwimu sinaonyesha kuwa Malaria iliwaua karibu watu nusu milioni duniani mwaka jana, huku vifo tisa juu ya kumi vikitoka kusini mwa Sahara.
Kenya ni miongoni mwa mataifa ya kusini mwa Jangwa la Afrika ambapo Malaria imeandelea kuangamiza watu lakini hali hii imeimarika  kwa asili mia nane ikilinganishwa na hali ilivyokua miaka sita iliyopita.
Isistoshe, wanawake waja wazito na watoto wako hatarini zaidi na wanatakikana  wanapokea matibabu punde zinapojitokeza dalili za ugonjwa kwani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni