Jumatano, 27 Aprili 2016

Mama Lucy KIbaki

Aliyekuwa mama wa taifa Aaga dunia


Baada ya kifo chake aliyekuwa Mama wa taifa nchini Kenya,watu wa tabaka mbali mbali wameendelea kutakia familia yake afueni,huku wakimumiminia sifa kama mama wenye bidiina aliyewajali wasiojiweza.

Juhudi zake za kuunda muungano wa akina mama wa marais afrika ili kukabiliana na ugonjwa wa ukimwi ni mfano wa mama aliyewajali wengine.

Pia alikuwa mstari wa mbele kuhakikisa maswala na afya ya uzazi imeimarishwa.Aliwatembelea wagonjwa hospitalini na aliyoyaona hasa mazingira mbaya wagonjwa waliokuwemo yalimtamausha.


Alinena kwa hasira na kutaka hatua kali zichukuliwe kwa maafisa wa selikali wafisadi .

Hospitali ya mama Lucy ilijengwa kwa heshima zake na wakaazi wa Embakazi wana sababu kushukuru kwa hayo."ukakamavu wake mama na bidii katika maswala la afya ilifanya sisi tupate hospitali karibu,tunafurahi sana,alisema Monica Wahito .

John Kariuki anasema ,''hospitali ya mama Lucy imekuwa na sifa mbaya ya kutekelezwa kwa waogojwa na jambo hili ni sharti libadilike kwa heshima ya mama Lucy Kibaki.
Alifanya mambo mengi ambayo tutamkumbuka.

Haijabainika alikokuwa akiugua .Kwa muda mrefu wakenya wamekuwa wakitaka kujua hatima yake ,kwani ajaoneka kwa miaka karibu sita.

Mama Lucy amekuwa akiuguakwa muda .Alilazwa katika hospitali moja hapa nchini Kenya hadi alipohamishwa jijini London kwa matibabu ya dharura hadi kufariki kwake hapo jana.

Mola ailaze roho yake mahali pema peponi.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni