Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Novemba, 2019

kongamano laicpd 25

Picha
Rais uhuru Kenyatta afungua rasmi Kongamano la idadi ya watu na maendeleo ICPD25 jiji Nairobi . Rais amehakikisha kuwa serikali ya Kenya itaweka mikakati ya kuhakikisha kuwa swala la ukeketaji wa wanawake limekabiliwa . Pia ametaka mataifa menginekuhakikisha haki za wanawake na jamii zinaheshimiwa. Upashaji tohara nchi na pia barani Afrika imekuwa ikiendelea licha ya hatua kali za kisheria dhidi ya wahusika. Kulingana na tafiti wanawake waliopashwa tohara wanakuwa  hatarini wanapojifungua huku wengine wakifariki wakati wa kujifungua.

ICPD 25 NAIROBI

Picha
Kongamana kuu la kimataifa limengoa nanga   nchini Kenya huku maswala ya afya ya uzazi yakiorodheshwa kuwa kipaombele kati ya maswala nyeti yatakayo jadiliwa. Isistoshe,malengo makuu tano yanayolengwa katika mjadala wa siku tatu wa kongamano la (ICPD25) ni kama vile ; haki ya afya ya uzazi,dhuluma za kijinsia na tabia tofauti ambazo zinaadhiri wanawake. Hata hivyo kuna baadhi ya vikundi ambavyo vina tofautiana na mkutano huu, hususan kuhusu maswala   ya uaviaji mimba na ngono za jinsia sawa yaani ushoga na ushagaji. Mashirika ya kidini yalipinga kuwa endapo maswala haya yatapewa nafasi ya kwanza, hawatahudhuria,huku wakisisitiza kuwa yanapinzana na desturi na mwelekeo wa dini. Vingozi wa dini wanakashifu hatua ya mkutano huu kwa kusema kuwa uaviaji mimba ni kitendo ambacho ni dhambi na pia ushoga hauna nafasi katika dini . Kwa mfano kanisa katoliki duniani hawaruhusu matumizi ya aina yeyote ya uzazi mpango hospitali wanazomiliki na zsisitiza ni dhambi. ...