Kongamana kuu la kimataifa limengoa
nanga nchini Kenya huku maswala ya afya
ya uzazi yakiorodheshwa kuwa kipaombele kati ya maswala nyeti yatakayo
jadiliwa.
Isistoshe,malengo makuu tano yanayolengwa
katika mjadala wa siku tatu wa kongamano la (ICPD25) ni kama vile ; haki ya
afya ya uzazi,dhuluma za kijinsia na tabia tofauti ambazo zinaadhiri wanawake.
Mashirika ya kidini yalipinga kuwa
endapo maswala haya yatapewa nafasi ya kwanza, hawatahudhuria,huku wakisisitiza
kuwa yanapinzana na desturi na mwelekeo wa dini.
Vingozi wa dini wanakashifu hatua ya
mkutano huu kwa kusema kuwa uaviaji mimba ni kitendo ambacho ni dhambi na pia
ushoga hauna nafasi katika dini .
Kwa mfano kanisa katoliki duniani
hawaruhusu matumizi ya aina yeyote ya uzazi mpango hospitali wanazomiliki na
zsisitiza ni dhambi.
Mwaka jana kasisi mmoja alikata kufanya
maombi ya wafu kwa mama aliyefariki na aliyedaiwa kuavya mimba.
Hata ikiwa maswala haya yanajitokeza wakati wa mkutano
huu,hakika ni kuwa kuna sababu za kiafya ambazo muunguzi anaweza kumshauri
mgonjwa kuavya mimba endapo maisha yake yatakuwa kwenye hatari.
Takwimu zilizotolewa zinaonyesha kuwa
Kenya ni miongoni mwa nchi sita ambazo zinaendelea kushamili katika maswala ya uzazi
mpango, huku idadi ya wanaotumia njia za kisasa za uzazi mpango ikiongezeka.
Ripoti
iliyozinduliwa mkabala na mkutano huu inaonyesha kuwa Kenya imepiga hatua
kukumbatia matumizi ya kondomu,sindano na vidonge.
Mkutano huu umeadaliwa na shirika la
idadi ya watu na serikali za Kenya na Denmark .
Mkutano kama huu ulifanyika Zaidi ya
miaka ishirini huko Cairo,Misri ambako azimio la Cairo lililatibiwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni