Alhamisi, 30 Januari 2020

Virusi vya Corona -WHO

Virusi vya Corona 
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza Virusi vya Corona kama dharura ya afya duniani.
Hii ni Kufuatia maafa ya kasi yanayotokea baada ya  mripuko wa maradhi ya virusi vya Corona.
Shirika la afya  ulimwenguni, WHO hiyo jana  lilifanya kikao cha kamati yake ya wataalamu  ili kujadili swala la iwapo kuna uwezaekano  kutangaza mripuko wa virusi vya Corona  kama dharura ya afya duniani.
Image result for international Health Regulations Emergency Committee on novel coronavirus in China
Kamati ya wataalamu Picha(WHO)
 watu zaidi ya 170 tayari wamefariki na zaidi ya wengine  elfu saba kuambukizwa tangu ulipotambuliwa mara ya kwanza jijini Wuhan, nchini China mwishoni mwa mwezi desemba ,mwaka wa 2019.

Mkutano huu ni watata kufanyika wiki hii .


Mkurugenzi mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Gebreyesus,akiadamana na watalam wa afya alizuru Uchina ilikutaadhmini hali ilivyo.Dkt. Gebreyesus anasema kusambaa kwa virusi hivyo hadi nje ya China ni tisho ambalo linatia hofu.

Virusi hivyo vinaenea kwa kasi na kufikia sasa mataifa mengi yameadhirika
Australia,Canada,Uchina,Ufaransa,Ugeremani,India,nepali,Korea Kusini na Marekani ni baadhi ya nchi zinazokabiliana na Virusi hivyo.

Wiki jana,WHO ilidokeza kuwa bado janga hilo halijafika kiwango cha kutangazwa dharura ya afya duniani.

Kulingana na wataalamu wa afya wanaohusika na tafiti za tiba ,chanjo ya virusi vya Corona inakisiwa  kuchukua Zaidi ya mwaka mmoja kukamilika.



Alhamisi, 23 Januari 2020

Corona Virusi


Serikali ya Kenya imetoa  tahadhari kubwa baada ya kesi ya virusi vya Corona kuripotiwa nchini China. 
Kupitia Kaimu mkurugenzi mkuu wa Wizara ya Afya Patrick Amoth ,serikali imesema tahadhari imetangazwa kwenye majimbo yote 47 kupitia Baraza la Magavana na wakurugenzi wa kaunti ya afya.
Pia ukaguzi na uthibiti umewekwa kwenye bandari na viwanja vya ndege nchini ili kukabiliana na hali hii.
 Nchi ya Uchina ina uhusiano mkubwa wa kibiashara na Kenya,huku wanabiashara na viongozi wa nchi wakisafiri kwenye nchi hizi mbili kila siku.
 "Kila siku, tunapata angalau ndege tatu hadi nne kwa hivyo tumeanza uchunguzi kwa abiria wote wanaokuja kutoka China," Amoth alisema.
Coronaviruses kawaida huathiri njia ya kupumua ya wanadamu na inahusishwa na homa ya kawaida, pneumonia na ugonjwa wa kupumua kwa papo hapo.
Dalili ni pamoja na homa, kukohoa na ugumu wa kupumua. Maambukizi ya virusi yanaweza kusababisha pneumonia  na virusi vinaweza kupitishwa kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine
Dkt Amoth alisema kuwa kufikia sasa, kesi 440 na vifo tisa vimeripotiwa. Aliongeza kuwa hivi ni virusi mpya  ambayo havijatambuliwa au kuripotiwa  hapo awali.
Ugonjwa huo umeenea hadi Beijing, na nchi zingine za Kusini-Mashariki mwa Asia kama Japan Thailand, Korea Kusini na kesi ya hivi karibuni iliripotiwa Marekani Jumanne. 
Shirika la Afya Ulimwenguni hapo awali lilikuwa limekataza uwezekano wa kesi kutambuliwa katika nchi zingine.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani, WHO Dkt Tedros Adhanom Ghebreyesus pia alifanya mkutano na wadau wa afya huko Geneva ili kutafuta mikakati ya kukabiliana na virusi ya Corona