Alhamisi, 30 Januari 2020

Virusi vya Corona -WHO

Virusi vya Corona 
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza Virusi vya Corona kama dharura ya afya duniani.
Hii ni Kufuatia maafa ya kasi yanayotokea baada ya  mripuko wa maradhi ya virusi vya Corona.
Shirika la afya  ulimwenguni, WHO hiyo jana  lilifanya kikao cha kamati yake ya wataalamu  ili kujadili swala la iwapo kuna uwezaekano  kutangaza mripuko wa virusi vya Corona  kama dharura ya afya duniani.
Image result for international Health Regulations Emergency Committee on novel coronavirus in China
Kamati ya wataalamu Picha(WHO)
 watu zaidi ya 170 tayari wamefariki na zaidi ya wengine  elfu saba kuambukizwa tangu ulipotambuliwa mara ya kwanza jijini Wuhan, nchini China mwishoni mwa mwezi desemba ,mwaka wa 2019.

Mkutano huu ni watata kufanyika wiki hii .


Mkurugenzi mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Gebreyesus,akiadamana na watalam wa afya alizuru Uchina ilikutaadhmini hali ilivyo.Dkt. Gebreyesus anasema kusambaa kwa virusi hivyo hadi nje ya China ni tisho ambalo linatia hofu.

Virusi hivyo vinaenea kwa kasi na kufikia sasa mataifa mengi yameadhirika
Australia,Canada,Uchina,Ufaransa,Ugeremani,India,nepali,Korea Kusini na Marekani ni baadhi ya nchi zinazokabiliana na Virusi hivyo.

Wiki jana,WHO ilidokeza kuwa bado janga hilo halijafika kiwango cha kutangazwa dharura ya afya duniani.

Kulingana na wataalamu wa afya wanaohusika na tafiti za tiba ,chanjo ya virusi vya Corona inakisiwa  kuchukua Zaidi ya mwaka mmoja kukamilika.



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni