Alhamisi, 27 Februari 2020

COVID -19 Kenya



Image result for kenya control coronavirusHuku ugonjwa wa Virusi vya Corona –COVID-19 ukiendele kuenea kwa kasi nje ya uchina ,Serikali ya Kenya imelaumiwa kwa kuruhusu kuingia nchini watu  239  warioabiri ndege ya Uchina.Inadaiwa kuwa abiria hao  walitakiwa wasikaribiane au wajitenge na watu kwa muda furani kama tahadhari dhidi ya kuambukiza wa Virusi vya Corona .
Hata hivyo kuna hofu kuwa huenda kunauwezekano kuwa mmoja au zaidi ya abiria wakawa na virusi hivyo ambavyo huchukua wiki kabla dhariri zake kuibuka.
Image result for kenya minister health coronaUgonjwa huu umewauwa maelfu ya watu nchini uchina na pia mataifa mengine nje ya Uchina yameadhirika.
Uchina umekuwa kitovu cha virusi, na kufikia sasa watu 81,291wameambukizwa vurisi hivi ulimwenguni kote na kuwauwa 2,770, wengi wao wakiwa katika taifa la Asia.
Image result for corona virusVirusi vya Corona ambao umepewa jina rasmi Covid-19, mara nyingi huenea kutoka kwa mtu mmoja hadi mtu.
Serikali kwa upande wake imesema hakuna haja ya kuhofia maambukizi kwani mikakati dhabiti imewekwa kuhakikisha hakuna mtu atakayeingia nchini bila kukaguliwa au kuchunguzwa iwapo ana virusi au la.
“Hatua zote za tahadhari zimewekwa na kila mtu anayekuja nchini hupimwa vya ipasavyo na watalamu wa afya.
Awali serikali ilisema kuwa mipaka na viwanja vya
ndege na pia bandarini hali imedhibitiwa.
Hata hivyo wakenya hawajaridhishwa na hatua ya serikali ya kutowarejesha wakenya 91 waliokwama nchini uchina.
Familia za wahusika sinasema kuwa wapendwa wao wamo hatarini yakuambukizwa virusi na pia kuadhirika kimawazo maana hawatoki nje na pia kuna upungufu wa chakula.
Kufikia sasa visa 15 vimefanyiwa tafiti kwenye mahabara kuhakikisha kuwa watu wote walioonyesha dalili za Corona wako salama.
·         Pia Mipango ya kuhamasisha umma kuhusu jinsi ya kukambiliana na virusi vya Corona endapo vitaripotiwa imewekwa.
·         Kitengo cha dharura chenye maafisa wenye majukumu ya kufatilia na kuchunguza kisa chochote kinachorioptiwa  nchini
·         Vifaa vya kutosha kuwekwa kwenye vituo maalum vya kuchunguza virusi kwa wasafiri wote wanaoingia nchini kutoka mataifa mbalimbali.
·         Mafunzo kwa maafisa wa afya huku maafisa mia tano wakifunzwa katika vituo vya afya vya umma na pia vya kibinafsi.
·         Wananchi wameshauriwa kuwashiriana na Wizara ya Afya kuripoti kisa chochote kinachshukiwa kuwa cha Corona.
Shirika la Afya Duniani lasema dunia sharti ijiandae kukambili na janga la virusi vya Corona
Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus anasema Virusi vya Corona vinaweza kuwa janga




Jumanne, 4 Februari 2020


Rais Mstaafu Daniel T Moi Aaga Dunia
Moi: The herdsboy who became Kenya's second president
Rais  mstaafu Daniel  Arap Moi ameaga dunia .


Mzee Moi  ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 95 katika hospitali ya Nairobi alipokuwa amelazwa tangu mwezi wa kumi mwaka jana.

Kundi la madaktari likiongozwa na Daktari wake wa miaka mingi, David Silverstein limekuwa likimpa mkatibabu kwa matatizo yanayojirejeeza na kumfanya kusalia kitandani kwa miezi mitatu.

Hali ya afya ya mzee Moi ilidorola Mwezi uliopita huku  madaktari wake  wakilazimika kumrejesha Moi katika chumba cha wagonjwa mahututi.

Kifo chake alfajiri ya leo kimetangazwa na Rais uhuru Kenyatta ambaye ni mwanafunzi na mwanawe wa kisiasaAwali,msemaji wake Lee Njiru  alisema Moi alikuwa amekwenda hospitali kwa ukaguzi wa kawaida wa afya lakini tangu wakati huo,amekuwa ndani nan je ya hospitali.
Mzee Moi, alijeruhiwa kwenye  goti alipohusika kwa ajari  iliyohusisha gari lake mwaka wa 2006 huko Limuru .


Moi alichukua hatamu za uongozi mwaka wa 1978,baada ya kifo cha Mwanzilishi waTaifa Marehemu Rais Jomo Kenyatta.


Kama mwandishi wa maswala ya afya nitamkubuka Rais Moi kama kiongozi aliyejari afya na malezi bora kwa watu hasa  watoto .Alihakikisha watoto walipata maziwa ya bure shuleni.


Pia alitilia mkazo mpango wa uzazi kwa akina na mama kwa minajiri ya afya bora na malezi mema.

Pia alijulikana kwa kuwa mtu aliyejali afya yake kwa kula vyakula vyene afya mwilini.

Kuhusu mazingira,Moi aliweka sera kuhakikisha wakulima wamepata miti ilikuzuia momonyoko wa udongo.


Alikuwa kwenye mstari wa mbele pia katika maswala la dini.

Rais alikuwa mkarimu, alipozuru sehemu tofauti za nchi aliwatunuku akina mama na watoto waliojitokeza kumlaki.

Pia alikuwa mcha Mungu.Kila jumapili rais hangekosa kanisani.


Mola ailaze roho ya Marehemu Rais Daniel Toritich Arap Moi palipo watakatifu wake.