Ijumaa, 18 Desemba 2020

chanjo ya Corona kwa wanafunzi

CHANJO DHIDI YA COVID -19


Tangu virusi vya Corona kutangazwa  kama janga la ulimwengu,sekta nyingi zimeadhirika hususan ile ya elimu.

 Watoto wanaostahili kuwa shuleni wamelazimika kusalia nyumbani huku serikali ikitafuka mbinu za kuhakikisha masomo yemerejelewa bila kuhatarisha Maisha ya Watoto.

 Nchini Kenya hatua mwafaka tayari zimeafikiwa kuhakikisha kuwa baadhi ya wanafunzi wamerejea shuleni huku wakihakikisha masharti ya kukabiliana  na Virusi ya Corona inapewa kipao mbele.

 Isistoshe,kuna haja  ya kuwachanja Watoto Pamoja na waalimu punde tu chanjo zitakapofika kwenye nchi mbalimbali duniani.

 Kulingana na taarifa za shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto, UNICEF chanjo dhidi ya COVID- 19 itakuwa hatua muhimu ya kurejesha hali ya masomo katika mstari wa kwanza.

Bi. Henrietta Fore, Mkurugenzi Mtendaji wa UNICEF anasema huku ugonjwa wa COVID-19 ukifika kilele na kupelekea shule kufungwa ,sekta ya elimu uliadhirika pakubwa huku asilimia 90 ya Watoto kote duniani wakibaki nyuma kimasomo.

Hata hivyo anashauri kuwa serikali zichukua hatua  kutoa chanjo kwa Watoto na wanaowatunza hasa walimu,baada ya wahudumu wa afya walio msitari wa mbele na makundi mengine yaliyo hatarini zaidi ya kuambukizwa COVID-19.

Ingawa kuna wale wanaohofia kurejea masomo kutahatarisha Maisha ya Watoto, Bi. Fore anasema kutofanya hivyo kutachangia Watoto wengi kukataa au kutoendelea na masomo katika umri mdogo na pia kwa wazazi wao kutoendelea na shughuli za kutafuta riziki -za kila siku.

Ingawa maamuzi ya kutoa chanjo hizo yako mikononi mwa serikali, “athari za kuendelea kukosa au kutohudhuria masomo ni kubwa sana hususan kwa watu wasiojiweza,amesema Bi. Fore.

Haya yanajili huku nchi ya Kenya ikitarajia kupokea chanjo dhidi ya virusi vya Korona kuanzia mwezi wa Januari mwaka wa 2021.

Chanjo hiyo ya Oxford University-AstraZeneca itawalenga Wahudumu wa afya, maafisa wa polisi, wakongwe na walimu.


Wengine watakao pata chanja kwa awamu ya kwanza ni wale ambao kazi zao zinawasabisha kuwa miongni mwa umati na wenye maradhi sugu ,imesema Wizara ya afya .

Waziri wa Afya Mutahi Kagwe, amesema kwamba Kenya itapokea chanjo milioni 24 kabla ya kushirikiana na kamapuni za taifa la Uchina.

Kagwe amesema kwamba Astrazeneca ni za bei nafuu ikilinganishwa na Pfizer ambayo  inastahili kuhifadhiwa katika mazingira ya -70° c.

Serikali inasema kuwa  Wakenya watapokea dozi hizo milioni 24 bila malipo kwani zimefadhiliwa na Shirka la Kitaifa la Chanjo GAVI.

 

 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni