Ijumaa, 18 Desemba 2020

Nyangarama Afariki Dunia-COVID

 Gavana Wa Jimbo La Nyamira Aaga Dunia

Gavana wa Kauti ya Nyamira John Obiero Nyagarama afariki dunia.

Nyagarama amekuwa akipokea matibabu katika Nairobi hospital iliyoko jijini Nairobi,kwa takriban mwezi mmoja.

Inasemekana Gavana Nyagarama alikuwa anaugua ugonjwa wa COVID-19.

Kulinagana na familia yake,alikuwa na matatizo ya kupumua baada ya mapafu yake kushindwa kufanya kazi.

Hata hivyo, Nyangarama amekuwa na matatizo ya kiafya ila familia yake imesita kusema alichokuwa anaungua .

Zaidi ya hayo, alisifika kwa kufanya miradi ya maendeleo kwenye kauti ya Nyamira, na pia kuwahimiza wakaazi umuhimu wa kujizuia kuambukizwa virusi vya Corona.

Pia
, alikuwa mkulima Hodari has awa zao la chai.Alifanya kazi katika sekta ya kilimo hususan majani chai na kupanda ngazi kwa kasi hasi akawa  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chai nchini kwa muda mrefu.

Hapo awali alifunza katika shule mbalimabli baada ya kufuzu kama mwalimu katika Chuo Kikuu cha Nairobi.Hadi kifo chake alikuwa na umri wa miaka 74.

Mola ailaze roho yake mahali pema peponi.

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni