Jumatatu, 11 Januari 2021

WHO UJUMBE -CHINA


WHO UJUMBE -CHINA

Uchunguzi uliosubiriwa kwa muda mrefu ili kujua kiini cha Virusi vya Corona ,Wuhan,China utaziduliwa hivi karibuni.

Hii ni kufuatia tanngazo kuwa Wanasayansi kumi wa Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) watatembelea Uchina kutoka Alhamisi.

Hii inakuja zaidi ya mwaka mmoja baada ya janga hilo kuanza.

Kumekuwa na mashtaka kwamba Beijing imejaribu kuzuia uchunguzikufanyika.

 Uchunguzi huu utakuwa muhumi ili kupata uvumbuzi wa chanzo cha janga la coronavirus ambalo limeharibu ulimwengu, na kusababisha vifo vya watu milioni mbili, na pia kupelekea kuzorota kwa uchumi wa ulimwengu.

 Ujumbe wa WHO utafanya utafiti wa pamoja na wanasayansi wa China juu ya asili ya Covid-19.

Hapo awali, Mkurugenzi Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus alikemea namna China ilikuwa ina chelewesha

Kuingia nchini kwa dakika ya mwisho ujumbe wake mapema mwezi.

 Haya hivyo,Wataalam wa WHO watalazimika kujitenga kwa wiki mbili baada ya kuwasili,Beijing.baadaye, wanatarajiwa kutembelea Wuhan - mji ambao virusi vya mauti viligunduliwa kwa mara ya kwanza mwishoni mwa 2019. 

Asili ya virusi

Amerika na Australia wamekuwa kwenye mtari  wa mbele kutoa wito wa kimataifa wa uchunguzi huru juu ya chimbuko la virusi, na kuiweka China chini ya shinikizo kubwa la uwajibikaji. 

Pia,Beijing imekabiliwa na ukosoaji wa kimataifa juu ya ukosefu wake wa uwazi wakati wa mlipuko wa mwanzo.

Wataalam watachunguza jinsi virusi viliruka kutoka kwa wanyama kwenda kwa wanadamu ili kuzuia janga jinginekutokea.Lakini udhibiti mkali unaotolewa na Uchina kuhusu utafiti wake wa kisayansi unadidimiza kupata suluhu kamili.

 Ni wazi kuwa virusi viliibuka mwishoni mwa 2019 kwenye soko moja huko Wuhan ambapo wanyama wa porini waliuzwa kama chakula.

Jaribio la kugundua asili yake pia limekumbwa na nadharia za njama - iliyoongezwa na Rais wa Merika Donald Trump - kwamba ilivuja kutoka kwa maabara ya virolojia ya Wuhan.

 


Jumatano, 6 Januari 2021

COVID-19 Kenya

 

COVID-19 Kenya waalimu

Huku chanjo dhidi ya Covid -19 ikitarajiwa kutolea baadaye mwezi wa Februari,serikali imesema kuwa  Walimu watapewa nafasi ya kwanza,miongoni mwa wafanyikazi wengine walioko kwenye hatari ya kupata maabukizi ya Covid-19.


 Hata hivyo,Wizara ya Afya inasema kuwa wanafunzi hawamo kwenye mpango wa chanjo kwa sababu majaribio ya chanjo ya kliniki kwa watoto bado hayajakamilika.

Awamu ya kwanza ya Zoezi la chanjo litalenga watoa huduma muhimu, pamoja na wafanyikazi wa afya na vikosi vya usalama.

Wazee na wale walio magonjwa mengine kama kisukali,shinikizo la damu,figo na mengine watapewa kipaumbele .

 Tangazo hilo lilitolewa na Katibu wakudumu katika Wizara ya Afya Dkt Mercy Mwangangi Jumatano.

 Alisema Kenya imepata dozi zake za kwanza milioni 24 za chanjo kupitia Covax, mpango wa nchi 189 ambao unakusudia kupata na kusambaza chanjo za Covid-19 kwa vikundi vilivyo hatarini ya maabukizi.

 Alisema Kenya hadi sasa imejaribu zaidi ya watu milioni moja dhidi ya  Covid-19 na imeweka mikakadi madhubuti kuzuia maambukizi ya coronavirus baada ya shule kufunguliwa Jumatatu wiki hii,nchini.

Hapo awali,Bi Henrietta Fore Mkurugenzi wa Shirika la umoja wa mataifa la watoto(UNICEF) alitaka selikali pia kutoa chanjo kwa wanafunzi na waalimu,ili kuzuia madhara kwenye sekta ya elimu.

Hata hivyo alisema uamuzi wa hatua hiyo uko mikononi mwa serikali husika.

 Takwimu zinaonyesha kuwa watoto hubaki bila dalili. Watoto kati ya miaka mitano na 19 hawako katika hatari kubwa ya kuambukizwa Covid-19 lakini wanaweza kubeba virusi na wanaweza kuambukiza watu wazima.

 Kenya ina zaidi ya walimu 340,000 wanaofanya kazi chini ya Tume ya Huduma ya Walimu (TSC) na karibu wengine 160,000 wanaofanya kazi katika shule za kibinafsi.

 Kumekuwa na hofu ya kuambukizwa kwa wingi mashuleni baada ya kufunguliwa Jumatatu baada ya fungwa tangu Machi mwaka jana.

kulikuwa na visa kadhaa vya walimu ambao walipata virusi hivyo na vifo vingine viliripotiwa,baadaya taasisi zilipofunguliwa mnamo Oktoba,mwaka jana.

 Kulingana na Dkt. Mwangangi Kenya itategemea sana chanjo ya AstraZeneca kwa sababu ya kubadilika kwake kwa mifumo ya sasa ya kuhifadhi baridi nchini.

 Pfizer na Moderna pia wameanzisha chanjo za Covid-19 lakini hizo zinahitaji kuhifadhiwa kwa joto la chini sana.Alitangaza kuwa wizara yake, pia itasambaza programu ya simu ya rununu,ijulikanayo kama M-Dharura ili kupata taarifa na pia kutoa habari kuhusu kesi za Covid-19.

 

WHO -China Ujumbe

 

China yawazuia wataalam wa afya wa WHO kuingia nchini humo.

Shirika la Afya Ulimwenguni(WHO) limekemea hatua ya Uchina,kuwazuia kuingia nchini humo kwa timu inayochunguza asili ya janga la coronavirus.

Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Dkt.Tedros Adhanom Ghebreyesus alisema wanasayansi wawili wa timu ya Umoja wa Mataifa tayari walikuwa wameondoka nchi zao kuelekea Wuhan, walipoambiwa kuwa maafisa wa China hawajapitisha idhini zinazohitajika kuingia nchini.

 Dkt.Ghebreyesus alisema alikuwa akiwasiliana na Uchina kabla ya ziara ya wawili hao kuanza, na kila kitu kilikuwa kamili baina yake na China.

Akihutubia wanahabari kutoka makao makuu ya shirika hilo,huko geneva,uswizi,Dkt.Ghebreyesus alisema,"Nimesikitishwa sana na habari hii."

 "Nimekuwa nikiwasiliana na maafisa wakuu wa China na nimeelezea kuwa ujumbe huu ni kipaumbele kwa WHO na timu ya kimataifa."

 azimio la kutaka uchunguzi huru.

Tedros alisisitiza kuwa madhumuni ya mkutano huo ilikuwa kutaadhmini hali hilivyo kuwa na kiini cha mripuko wa coronavirusi,kama ilivyopi asimiwa na mataifa mia moja ,mei mwaka uliopita.

 Hapo awali, uchina ilikuwa imewahakikishia kuwa ilikua kwenye harakati za kujiadaa kupokea ujumbe huo.

Maafisa wa WHO kwa muda mrefu wamekuwa wakifanya mazungumzo na Beijing kuruhusu timu ya wanasayansi wake kupata fursa kuchunguza asili ya virusi – vilivyo gunduliwa kwanza huko Wuhan mnamo Desemba 2019.

 Katika mkutano na waandishi wa habari Jumatano, msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje ya China, Hua Chunying, alisema Uchina imekuwa na mtazamo wazi, uhuru na uwajibikaji kila wakati katika harakati za kutafuta asili ya coronavirusi.

 Hua alisema,hapo awali nchi yake,ilikuwa imekaribisha wataalam wa WHO nchini na akasema kuwa timu ya uchunguzi ya Umoja wa Mataifa na wataalam wa China wakuwa na ushirikiano wa mara kwa mara.

 Alisema,ili kuhakikisha kuwa kikundi cha wataalam wa kimataifa kinachokuja China kinaweza kufanya kazi vizuri, inahitajika kutimiza taratibu zinazohitajika na kufanya mipango maalum inayofaa.

Beijing imekuwa ikiishutumiwa jinsi inavyochukulia swala hili hasa katika kuchunguza kiini za maambukizi ya virusi vya COVID 19.

Hii imepelekea uhusiano wake na marekani kuzorota.

Rais wa Merika Donald Trump amekuwa akilaumu China mara kwa mara kwa kuregea kwake kukabili janga hili.

Kufuatia uhusiano mbaya kati ya nchi hizi mbili,Marekani itasitisha uhusiano wake na WHO, ikisema kuwa Uchina haikuripoti habari sahihi iliyokuwa nayo juu ya coronavirus na ilishinikiza WHO "kupotosha ulimwengu."

Marekani imetaka uwazi katika shughuli za WHO nchini China.

 Pia inadaiwa kuwa maafisa wa China walitoa habari za kupotosha kuhusu idadi ya kesi wakati wa hatua za mwanzo za mlipuko wa Virusi ya Corona.

 

Jumanne, 5 Januari 2021

Oxford-AstraZeneca

 Chajo ya Oxford-AstraZeneca

Huku chanjo dhidi ya virusi ya Corona yaani COVID -19 ikianza kutolewa kwenye mataifa yalioendelea,kenya inatarajiwa kuanza kutoa chanjo hiyo mwanzoni mwa januari mwaka huu.

Hapo awali, Wizara Ya Afya ilitoa taarifa kuwa Shehena ya chanjo ya Covid-19 inatarajiwa nchini Kenya mwezi huu, huku walengwa wa kwanza wakiwa vikundi vilivyo katika hatari kubwa ya kuambukizwa virusi.

Isitoshe,Kenya imeagiza  dozi milioni 24 za chanjo ya Chuo Kikuu cha Oxford-AstraZeneca ambayo ni ya bei nafuu na inahifadhiwa kwa urahisi.

Baadhi ya walio kwenye hatari ya maambukizi ya virusi vya Corona ni pamoja na Wafanyikazi wa afya, maafisa wa polisi, wazee na walimu .

Chanjo ya Chuo Kikuu cha Oxford-AstraZeneca itatolewa  katika robo ya kwanza ya mwaka huu.

Kulingana na Wizara ya Afya watu ambao wanaokuwa kwenye mukushanyiko wa umati na wale walioadhirika na magonjwa mengine ya kiafya watakuwa wa kwanza kupewa chanjo dhidi ya coronavirus.

Inakadiriwa asilimia 20 ya idadi ya watu nchini watapokea chanjo katika awamu ya  kwanza.

Zaidi ya hayo, serikali inachunguza njia za kushirikiana na mashirika mengine kama yale ya Wachina ambayo yameunda vidonda vya Covid-19 na wengine.

Kwa sasa,Kwa sasa, Chanjo tatu ambazo zimefanyiwa utafiti dhidi ya COVID-19 ni ile ya Chuo kikuu cha Oxford inayojulikana kama AstraZeneca ,Pfizer’s kutoka kwa kampuni ya kutengeneza 

madawa na Moderna inayotolewa kwa matumizi ya dharula.