Ijumaa, 26 Machi 2021

Reuben Githinji

 

Reuben Githinji

Ugonjwa wa COVID-19 umetupokonya mwanadishi aliyebombea Reuben Githinji.

Githinji aliugua na alihitaji dharula lakini hospitali ya mkoa ya Embu,haikuwa na nafasi.

Ilibidi ahamishe hadi Hospitali ya Muranga ambapo alifariki akipokea matibabu.

Nimehuzunishwa na kifo cha mtu niliye mfahamu kwa muda mrefu na nilimuita kakangu.

Nilikutana naye Reuben Githinhji alipokuwa anandkikia kampuni ya Kenya Times huko Meru.

Nilikuwa mwandishi wa Habari aliyekuwa anajifunza uanahabari,hivyo basi baadaya ya rikizo kutoka chuoni tulitakiwa kutafuta nafasi ya miazi nne ili kufijunza nje ya darasa.

Kwa bahati nzuri, nilipata nafasi kutoka kwa kampuni ya nation wakanituma, wilaya ya Meru alipokuwa mwanahabari wao Imanene Imathiu ambaye ni marehemu.

Katika harakati za kukusanya Habari hapa ana pale nilikutana na Githinji ambaye alikuwa anapenda sana kazi yake.

Alipenda sana kuandika kuhusu maswala ya siasa na jamii kwa jumla.

Nkumbuka wakati ule Kampuni ya Kenya Times ilikuwa inachelewa sana kuwalipa wafanyakazi wake lakini yeye hakukata tamaa.Alijitolea kufanya kazi kwa moyo wake wote.

Hadi Kenya Times walipofunga na akajiunga na Kampuni ya Nairobi Star amekuwa mwanahabari mkakamavu aliyependa kufanya kazi yake bila kusukumwa.

Waliofanya kazi naye watasema kuwa alipanda milima na mabonde kutafuta Habari na Makala ambayo ingebadilsha sura ya jamii alimoishi hasa katika majimbo ya Meru na Embu.

Ingawa tulitumikia kampuni tofauti,tuishi kama familia moja na kusaidiana katika maswala ya uanahabari.

Mola ailaze roho yake pema peopni…..

Githinji lala salama.

Chebet Karago

Lala salama Chebet

Tangu utotoni,ilikuwa ni ndoto yangu kuwa mwanahabari mashuhuri.

Hakika nilipenda sana kuwa mwanahabari.

Ndoto yangu ilitimia nilipopata fursa ya kujiunga na Chuo cha Mawasilisano na Utangazaji, K.I.M.C, maeneo ya South C.

katika halakati ya masomo,tulitakiwa kutafuta moja wapo ya mashirika au kampuni zinazo chapisha na pia kutangaza habari na matukio tofauti nchi na duniani kwa ujumla.

Baada ya kufikiria kwa muda,niliamua kwenda katika kituo cha habari cha Nation.

Hapo ndipo nilikutana na wanahabari waliobobea kama vile Caleb Atemi, Marehemu Bob Okoth,Amos Ngaira,Njeri Rugene baadhi wa wanahabari wengine.

Aliyenipokuwa hasa kwa mikono miwili alikuwa ni mwendazake Chebet Karago ambaye alinielekeza jinsi ya kuwa mwanahari na kunisaidi sana katika nyaja ya uwanahabari.

Mkutano na Chebet.

Nilikutana na mwandishi Chebet Karago katika jumba la Nation, nilipokuwa nimeenda kuomba nafasi ya kuandika katika gazeti la Sunday Nation hasa kwenye ukurasa wa Young Nation.

Nipofika nikaelekezwa alipokuwa ameketi .Alinikaribisha kama rafiki aliyemfahamu kwa muda mrefu.

Isitoshe,alinisikiza kwa makini nilivyo jieleza na baadaye akaniuliza ikiwa nina Makala ningetaka tuchapishe,kukahikisha nilikuwa na uhakika

 Hivyo basi,Nilitoa Makala niliyokuwa nimechapisha hapo awali chuoni na nikamkabidhi ,akaipokea na kaniahidi kuwa yuko tayari kuchapisha habari zangu.

Wiki iliyofuatia nilifurahi sana kusoma makala yangu kuhusu Shem Chusia ambaye nilimhoji baada ya kutunukiwa zawadi na Shirika la Utangazaji la BBC, alipoimbuka mshindi wa makala maalum ya vipindi vya uigizaji vya radio.

Kutoka hapo akanitia shauku ya kutaka kuendelea kuandika.

Pia,nilikuwa ninaandika makala kwenye gazeti la Taifa Leo baada ya kupewa fursa na aliyekuwa Mkurugenzi wa Taifa Leo marehemu Bob Okoth.

Hakika,Chebet alikuwa mwanahabari, mwenye maneno machache lakini ulipozungumza naye alisikiliza kwa makini.Mwenye upendo hususan kwa maswala ya akina mama na watoto.Pia alikuwa mwenye mitindo.

Alikuwa mama mpenda watu,mwenye mavazi ya kimitindo na asiyemwingi wa maneno.aliye andika kwa ustadi-Gwiji .

Fauka ya hayo,alinishika mkono kama dadake na kuhakikisha kuwa ninaandika kulingana na kanuni zilizoko za uanahaba.Asante sana Chebet kwa nafasi uliyonipokeza.

Mola ailaze roho yako mahali pema walalapo watakatifu.Amina