Lala salama Chebet
Tangu
utotoni,ilikuwa ni ndoto yangu kuwa mwanahabari mashuhuri.
Hakika
nilipenda sana kuwa mwanahabari.
Ndoto
yangu ilitimia nilipopata fursa ya kujiunga na Chuo cha Mawasilisano na Utangazaji,
K.I.M.C, maeneo ya South C.
katika
halakati ya masomo,tulitakiwa kutafuta moja wapo ya mashirika au kampuni zinazo
chapisha na pia kutangaza habari na matukio tofauti nchi na duniani kwa ujumla.
Baada ya
kufikiria kwa muda,niliamua kwenda katika kituo cha habari cha Nation.
Hapo ndipo
nilikutana na wanahabari waliobobea kama vile Caleb Atemi, Marehemu Bob
Okoth,Amos Ngaira,Njeri Rugene baadhi wa wanahabari wengine.
Aliyenipokuwa
hasa kwa mikono miwili alikuwa ni mwendazake Chebet Karago ambaye alinielekeza
jinsi ya kuwa mwanahari na kunisaidi sana katika nyaja ya uwanahabari.
Mkutano na Chebet.
Nilikutana
na mwandishi Chebet Karago katika jumba la Nation, nilipokuwa nimeenda kuomba
nafasi ya kuandika katika gazeti la Sunday Nation hasa kwenye ukurasa wa Young
Nation.
Nipofika
nikaelekezwa alipokuwa ameketi .Alinikaribisha kama rafiki aliyemfahamu kwa
muda mrefu.
Isitoshe,alinisikiza
kwa makini nilivyo jieleza na baadaye akaniuliza ikiwa nina Makala ningetaka
tuchapishe,kukahikisha nilikuwa na uhakika
Hivyo basi,Nilitoa Makala niliyokuwa
nimechapisha hapo awali chuoni na nikamkabidhi ,akaipokea na kaniahidi kuwa
yuko tayari kuchapisha habari zangu.
Wiki
iliyofuatia nilifurahi sana kusoma makala yangu kuhusu Shem Chusia ambaye
nilimhoji baada ya kutunukiwa zawadi na Shirika la Utangazaji la BBC,
alipoimbuka mshindi wa makala maalum ya vipindi vya uigizaji vya radio.
Kutoka
hapo akanitia shauku ya kutaka kuendelea kuandika.
Pia,nilikuwa
ninaandika makala kwenye gazeti la Taifa Leo baada ya kupewa fursa na aliyekuwa
Mkurugenzi wa Taifa Leo marehemu Bob Okoth.
Hakika,Chebet
alikuwa mwanahabari, mwenye maneno machache lakini ulipozungumza naye alisikiliza
kwa makini.Mwenye upendo hususan kwa maswala ya akina mama na watoto.Pia
alikuwa mwenye mitindo.
Alikuwa mama
mpenda watu,mwenye mavazi ya kimitindo na asiyemwingi wa maneno.aliye andika
kwa ustadi-Gwiji .
Fauka ya
hayo,alinishika mkono kama dadake na kuhakikisha kuwa ninaandika kulingana na
kanuni zilizoko za uanahaba.Asante sana Chebet kwa nafasi uliyonipokeza.
Mola ailaze
roho yako mahali pema walalapo watakatifu.Amina
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni