Jumanne, 21 Mei 2024

 

Ugonjwa Wa Pid

Ugonjwa huu husababishwa na magonjwa ya zinaa kama vile kisonono (gonorrhea) na pangusa (chlamydia). mwili wa mwanamke unapokuwa na afya njema, mlango wa kizazi huwa na uwezo mkubwa wa kuzuia bakteria wasiweze kuingia katika viungo vya ndani vya uzazi kutoka ukeni.Hata hivyo wakati mlango wa kizazi unabukizwa na magonjwa ya zinaa hasa kisonono (gonorrhea) na pangusa (chlamydia), mlango wa kizazi hupoteza uwezo wake na hivyo kuruhusu maambukizi na bakteria kuingia na kufika juu kwenye viungo vya uzazi.Zaidi ya hayo,kuna njia kadhaa ambazo mwanamke anaweza kuambukizwa ugonjwa wa pid. njia hizo ni kama vile:

 Kuwa na  ugonjwa wa zinaa na hujatibiwa;kufanya ngono na wanaume tofauti bila kutumia mpira au kodomu kujizuia; mwanamke aliye na historia ya kuugua pid hapo awali;maambukizi je ya uzazi baada ya kuavya mimba au baada ya mimba kutoka (miscarriage);maambukizi ya nje ya uzazi hasa baada ya ama kujifungua

 Dalili za pid kwa mwanamke

Kuna dalili kadhaa za ugonjwa wa pid kwa mwanamke, miongoni mwa dalili hizo ni kama vile:

 kuhisi maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chini ya kitovu.

kupata maumivu ya mgongo.

kutokwa na  mchafu ulio na harufu mbaya kwenye sehemu za siri.

kuhisi maumivu wakati wa kukojoa.

kupata maumivu na kutokwa na damu wakati wa tendo la ndoa. 

 kupata homa.

kuhisi kichefuchefu na kutapika.

 Matibabu ya pid

 Matibabu ya pid ni  kutumia dawa  hasa za antibiotics .daktari humtaka mogonjwa apewe dawa inayoendana na chanzo cha tatizo lako.huku ukipewa nafasi ya mud awa  siku kama tatu kuona kama dawa zinafanya kazi kama inavyotarajiwa.dawa za pid zinazotolewa na daktari ni metronidazole tabs, doxycycline tabs na cefixime tabs

 mume au mpenzi pia anastahili kutibiwa kuepuka kusambaa tena baada ya matibabu.pia ni muhimu kuacha kushiriki ngono kwa muda.hasa kuacha kushiriki ngono hadi utakapomaliza tiba na kuona kuwa umepona.

 madhara ya pid enapo hayatatiziwa

 PID ambayo haikupata tiba inaweza kusababisha makovu na vifuko vyenye maji yenye wadudu kwenye mkondo wa njia ya uzazi ya mwanamke, vitu hivi vinaweza kusababisha madhara ya kudumu kwenye viungo vya uzazi. madhara yanayoweza kutokea kama mimba nje ya mirija ya uzazi (ectopic pregnancy). pia pid ndiyo sababu ya mimba kutunga nje ya kizazi, mimba huweza kutunga nje ya kizazi endapo pid imesababisha makovu ndani ya mirija ya uzazi. makovu haya husababisha yai lililopevushwa kushindwa kusafiri ndani ya mirija ya uzazi kuelekea kwenye nyumba ya mirija ya uzazi. mimba nje ya uzazi husababisha utokaji wa damu usiowakawaida unaoweza kukatisha maisha ya mwanamke.

 Utasa

Viungo vya uzazi vinapoharibikakuna uwezekano mkubwa  kusababisha utasa, kushindwa kupata ujauzito. endapo mama atazidi kupata pid mara nyingi zaidi basi atakuwa kwenye hatari ya ugumba na pia  kuchelewa kupata tiba ya pid kuongeza hatari ya ugumba.

PID inaweza kusababisha maumivu ya nyonga yanayoweza kudumu kwa muda mrefu. makovu ndani ya mirija ya uzazi na viungo vingine vya uzazi huweza kulsambabisha maumivu wakati wa kujamiiana na wakati yai huondoka (ovulation).

Isitoshe,Pid huwa na madhara megi kwa akina mama maana  usababisha kuwepo kwa usaha na kufanya majipu ndani ya mirija ya uzazi na ovari, huku kuleta maambukizi hatarishi kwa maisha.mama mja mzito hupata madhara mengi endapo atashindwa kupata tiba ya pid mapema.madhara yaliyo ripotiwa ni kama vile; kujifungua kabla ya wakati au ujauzito kuharibika;  kujifungua mtoto mwenye maambukizi na wakati mwingine hufariki muda mchache baada ya kujifungua au kujifungua mtoto mfu; kuziba kwa mirija ya uzazi.

 kuna njia tofauti kuzuia ugonjwa huu kama vile;

 kutembelea viyuo vya afya mara kwa mara au wakati dalili zinapojitokeza kupima na kufuata maagizo ya wataalamu wa afya .pia wakati unapogundua kuwa mpenzi wako ana dalili za magonjwa ya zinaa au anajamiiana  na wanawake wengi.kufanya vipimo mara kwa mara hasa vipimo vya uzazi, pamoja na vipimo vya maambukizi ya magonjwa yanayosambazwa ka njia ya ngono (sti) hususani kwa mgonjwa wa chlamydia, ufanye vipimo kila mwaka mara moja.

Hivyo basi ni uhimu pia,kutofanya ngono mara baada ya kujifungua, mimba kutoka au mara baada ya kutoa mimba ili kuhakikisha njia ya shingo ya uzazi imefunga vyema.lakini njia muhimu ni hakikisha  kujizuia na maambukizi kwa  kuacha ngono bila kuvaa kodomu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni