endometrial cancer-Saratani ya uterazi
Saratani ya shingo ya uzazi bado ndiyo aina ya kansa ya uzazi inayoshababisha maafa ya akina mama zaidi nchini Kenya. Takwimu kutoka Kenya Cancer Registry zinaonyesha kwamba zaidi ya wanawake 5,200 hugunduliwa kuwa na saratani ta Uterine kila mwaka, na hiyo ni karibu asilimia 20 ya wanawake wote wanaopata ugonjwa huo.Inasikitisha kuwa zaidi ya wanawake 3,200 hufa kila mwaka, hii ikiwa sababu kuu ya idadi kubwa ya vifo vinavyohusiana na saratani miongoni mwa wanawake, ya pili baada ya kansa ya matiti inayoongaza.
Kulingana
na wataalamu wa afya saratani ya shingo ya uzazi inaweza kuzuiwa kwa
uchunguzi wa kawaida na chanjo ya HPV, hii inaweza kupunguza
visa vingi vya magonjwa haya, anasema Dk. Gladys Mugambi, afisa mwandamizi wa
Wizara ya Afya. Mugambi
anasema shughuli ya kutafuta chanjo na wagonjwa bado ni ya chini sana, hasa
katika maeneo ya vijijini.
Mojawapo ya changamoto kubwa za Kenya ni
kugunduliwa kwa magonjwa . Uchunguzi unaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 90 ya
wanawake hupatwa na ugonjwa huo lakini wanatafuta matibabu ya afya baadaye, wakati ugonjwa umeenea Zaidi.Zaidi ya hayo, matibabu ni magumu kepata bila pesa kwani ni ghali.
Tafiti
zinaonyasha kuwa ni asilimia 14-18 tu ya wanawake wa
Kenya wenye umri wa kati ya miaka 18 na 69 ambao wamewahi kuchunguzwa endapo wanaugua saratani ya kizazi, hki ni kiwango cha chini sana kilingana
na malengo ya WHO la kufikia asilimia 70 ya uchunguzi
kufikia mwaka 2030.
Hali ni mbaya sana katika kaunti kama vile Kisumu,
ambapo chini ya asilimia 6 ya wanawake walipimwa mwaka 2019. Mara kwa mara, vituo
vya afya havina vifaa vya kugundua ugonjwa huo mapema, na bado wanawake wengi
hawaendi kwenye vituo vya uchunguzi kwa sababu ya ubaguzi wa kitamaduni au vituo vya afya viko mbali na
makao yao.
| picha ya Cleveland Clinic |
Kansa ya ovari: takwimu zinaonyesha kuwa kuna visa nyingi ulimwenguni.Karibu visa vipya vilivyo ripotiwa ni kama vile; 90,000 mnamo
2022, na zaidi ya vifo 32,000. Nchini Kenya, kiwango cha kuudhibiti chaendelea
kuwa cha chini kwa sababu ya ukosefu wa matibabu maalum. Saratani ya
kizazi (endometrial), Ilirekodiwa visa vipya 60,000 ulimwenguni kote mnamo 2022, lakini eimu au uhamazisho kuhusu saratani
hii ni mchache nchini Kenya .
Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO) linasema
kwamba zaidi ya asilimia 90 ya vifo vinavyotokana na saratani ya kibofu
hutokea katika nchi zenye mapato ya chini na ya kati. Chanjo ya HPV, ambayo sasa
inapatikana nchini Kenya kwa wasichana wenye umri wa miaka 10-14 ina uwezo wa
kupunguza kwa kiasi kikubwa maambukizi mapya iwapo kiwango cha maambukizi
kitaongezeka.
Hata hivyo, maendeleo hayafanyiwi kwa
usawa. Katika maeneo fulani ya mashambani, habari za kupotosha ,tamaduni na mila kuhusu chanjo zimedhoofisha
kampeni za chanjo. Wakati huohuo, miundombinu ya uchunguzi na matibabu ingali
imejikita katika vituo vya mijini kama Nairobi na Mombasa, na kuwaacha wanawake
katika maeneo ya mbali kuwa hatarini.
Mikakati
ya kudhibiti saratani
Kenya imepitisha mkakati wa Kimataifa wa
WHO wa kuukabili
ugonjwa wa Saratani ya Shingo ya Uzazi, ambao unaweka
malengo makubwa kama
vile;
·
Asilimia 90 ya wasichana
wamechanjwa kabisa dhidi ya HPV kufikia umri wa miaka 15
·
Asilimia 70 ya wanawake
kuchunguzwa angalau mara mbili katika maisha yao
·
Asilimia 90 ya wanawake walio
na ugonjwa wa kabla ya kansa au kansa wanaopokea matibabu
Kutimiza malengo haya itahitaji uwekezaji
mkubwa, kampeni za uhamasishaji, na kuvunja ukimya kuzunguka afya ya uzazi.
"Ugonjwa wa saratani ya kizazi si
suala la matibabu tu, ni suala la haki ya kijamii", anasema Dkt. Esther
Mwaura, mtetezi wa afya ya uzazi. Anasema hakuna
mwanamke anayepaswa kufa kutokana na ugonjwa ambao tayari tunajua jinsi ya
kuuzuia.
Hatua muhimu
Kadiri visa vya saratani vinavyoongezeka,
wataalamu wanaonya kwamba kunyamaza na unyanyapaa kunaweza
kusababisha kifo. Kutoa
elimu and kuendelea na chanjo ya HPV, kuongeza mipango ya
uchunguzi, na kuimarisha vituo vya huduma ya saratani ndiyo njia muhimu ambayo Kenya inaweza kukabiliana na hali hiyo.
Kwa sasa maelfu ya wanawake na wanaume, wako kwenye hatari endapo hatua za
dharula za kuudhibiti ugonjwa huu hazitachukuliwa.
Maoni
Chapisha Maoni