MPOX nchini Kenya
Wakati Wizara ya Afya ya Kenya
ilipothibitisha visa vya kwanza vya maradhi ya mpox ,iliyokuwa ikijulikana
kama monkeypox mwezi Julai 2024, watu wengi hapa nchini walishanga kwa sababu ,hawakuwa na
Habari kuhusu ugonjwa huo ambao ,unasemekana kuenea katika Afrika ya Kati.
Kwa vyovyote vile, ugonjwa wa Mpox.
Wakenya wafikiri
huu mi ugonjwa wan Ndui au smallpox ambao uliangamizwa
ulimwenguni pote mwaka wa 1980.Isitoshe, kumekuwa na hofu huku
wengi wakishagaa kwa nini tunasikia kuhusu virusi vya ndui
tena?
Ukweli ni kwamba mpox imekuwapo kwa miongo
mingi, lakini hadi hivi majuzi ilionekana hasa katika Afrika ya Kati na ya
Magharibi. Kwa sas visa vya ugonjwa huo vimeripotiwa katika nchi kadhaa za Afrika Mashariki hususani Kenya.
Mpox huenea vipi?
Mpox husababishwa na virusi vya familia ya ndui au smallpox. Inasambazwa kupitia mahusiano ya karibu yaani ngozi kwa ngozi, umajimaji wa mwili, nyuso zilizochafuliwa, na wakati mwingine kutoka kwa wanyama hadi kwa wanadamu.
Zaidi ya
hayo, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imekuwa
kitovu cha maambukizi
haya kwa miaka
mingi. Kati ya mwaka 2023-2024, nchi hiyo
iliripoti zaidi ya visa 14,000 vya wagonjwa na vifo zaidi ya 650. Variant au virusi yenye nguvu zaidi, iitwayo clade Ib, imefanya mambo yawe mabaya
zaidi, ikisambaa kwa kasi mno na kushambulia kwa nguvu zaidi. Bali na DR Congo, ugonjwa huo umeenea hadi nchi jirani kama vile Burundi na Jamhuri
ya Afrika ya Kati.
Matukio ya kwanza Kenya
Mnamo Julai 2024, Kenya ilithibitisha visa
viwili vya kwanza vya mpox katika Kaunti ya Taita Taveta. Mgonjwa mmoja alitoka Kaunti ya Kiambu, wakati mwingine alikuwa raia
wa Kongo. Kwa kusikitisha, majuma machache baadaye, inadaiwa kuwa Kenya
ilirekodi kifo chake cha kwanza kinachohusiana na mpox, mtu anayeishi na virusi
vya UKIMWI ambaye alipata matatizo makubwa.
Kufikia mapema mwaka 2025, Kenya ilikuwa
imethibitisha visa 33 katika kaunti 12, na maafisa wa afya walikuwa
wamefuatilia zaidi ya watu 200 waliowasiliana na virusi hivyo. Wengi wa
maambukizi walikuwa wanaohusishwa na madeleva wa lori ambao husafiriki kutoka nchi za Afrika mashariki hadi
Nchi ya DR Congo na pia vituo vya mijini ambapo watu hujumuika kwa wingi.
Kulingana na Wizara ya Afya ,Kenya ,Kaunti
ya Mombasa ina idadi kubwa zaidi ya maambukizi kwa 146, ikifuatiwa na Busia na
maambukizi 63, Nakuru (21), Kilifi (19), Nairobi (17), na Makueni (13).
Taita-Taveta na Uasin Gishu wamerekodi visa vitano kila mmoja, wakati Bungoma
ina visa vinne. Kajiado, Kakamega, na Kiambu kila moja imeorodhesha maambukizi
matatu.
Hadi sasa, kulingana na takwimu, watu nchini Kenya ni wachache sana ambao wamepatikana na ugonjwa huo ikilinganishwa na DRC. Lakini wataalamu wanaonya kuhusu changamoto kadhaa kama vile
Uchunguzi mdogo: Uchunguzi wa mpox chini ya 500 ulifanywa katika miezi saba ya
kwanza, ikimaanisha kuwa visa vingine havijatambuliwa.
Ufahamu mdogo: Watu wengi bado wanachanganya mpox na ndui au smallpox wanafikiri
kwamba huathiri vikundi fulani tu. Hilo hupunguza namna au hali ya kutafuta matibabu ya kiafya na pia kutoa ripoti kuhusu maambukizi.
Unyanyapa: Kama ilivyokuwa wakati virusi vya UKIMWI vilipoanza, familia fulani huficha watu wa ukoo walio wagonjwa kwa kuogopa kuhukumiwa na jamii , jambo ambalo linaweza kufanya ugonjwa huo kueneea zaidi.
Mbinu za
kukabiliana na Mpox
Ni muhimu
kwa nchi kuchukua hatua mwafaka ili kuudhimiti ugonjwa huo.Kenya imeongeza ukaguzi wa mipaka, imeweka tahathali za
kusafiri, na kampeni za uhamasishaji wa umma. Jambo la muhimu ni kwamba, Kenya imefanya
mipango ya kutoa chanjo kwa mikoa, na pia Shirika la Afya Duniani(WHO) na washirika wake wamejiandaa kutoa dozi 50,000 za chanjo ya mpox
kwa matumizi nchini Kenya na nchi nyingine za Afrika.
Maafisa wa afya wanasema chanjo hiyo
itapelekwa kwanza kwa wafanyikazi wanaofanya na mashirika ya afya au wahudumu wa afya, watu wenye kinga dhaifu, na makundi wenye kuwa hatarini kama vile madereva
wa malori ambao husafiri kwa
kuvuka mipaka.
Ingawa Mpox sio mpya, lakini kuenea kwake nchini Kenya ni ukumbusho kwamba
magonjwa ya kuambukiza hayana mipaka. Habari njema ni kwamba Kenya inaweza
kujifunza kutokana na mapambano ya ulimwenguni kote dhidi ya ndui au smallpox:
kwa kutumia mbinu kama chanjo, elimu, na
ufuatiliaji, hali inaweza kubadilika.
Kwa sasa, umuhimu ni kuwa na ufahamu. Kujua dalili kama vile - homa, maumivu ya mwili, kuvimba kwa lymph
nodes, na upele unaogeuka kuwa vidonda vilivyojaa maji - kunaweza kuwasaidia
watu kutafuta matibabu mapema na kuepuka kueneza virusi.
Mlipuko wa mpox nchini Kenya bado ni mdogo,
lakini ni sehemu ya hadithi kubwa zaidi ya kikanda. Kwa kuwa Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo inakabiliwa na maelfu ya visa, na nchi jirani zinaripoti
milipuko yao ya kwanza, inadhibitisha
kuna hatari ambayo sharti ikabiliwe mapema.
Kama vile ugonjwa wa ndui ulivyoshambuliwa
kwa jitihada za pamoja, mpox pia inaweza kudhibitiwa ikiwa tunawekeza katika
afya ya umma, ushirikiano wa mipaka, na ufahamu wa jamii.
Maoni
Chapisha Maoni