Machapisho

TB day

Siku ya Kifua Kikuu Duniani Siku ya Kifua Kikuu (TB) Duniani huamasishwa Machi 24kila mwaka.lengo likiwa kufahamisha umma idadi ya maabukizi,vifo, juhudi za kukomesha janga la TB na binu mpya zinazobuniwa ili kukabiliana na makali ya ugonjwa wa TB. Mnamo Tarehe mwaka wa 1882 Dk Robert Koch alitangaza kwamba amegundua bakteria inayosababisha TB, ambayo ilitoa fursa ya kutambua na kuponya ugonjwa huu. TB inasalia kuwa moja ya magonjwa hatari zaidi ya kuambukiza ulimwenguni. Kila siku, zaidi ya watu 4100 hupoteza maisha kwa TB na karibu watu 28,000 wanaugua ugonjwa huu unaozuilika na pia kutibika. Juhudi za kimataifa za kukabiliana na TB zimeokoa maisha ya takriban milioni 66 tangu mwaka wa 2000. Hata hivyo, janga la COVID-19 limerudisha nyuma maendeleo ya miaka mingi iliyopatikana katika vita vya kukomesha TB. Kwa mara ya kwanza katika zaidi ya muongo mmoja, vifo vya TB viliongezeka mwaka 2020. Kauli mbiu ya Siku ya Kifua Kikuu Duniani mwaka huu-2022, ni ‘Wekeza Kukomesha Kifua K...

COP26 Glasgow,Scotland

Picha
         Viongozi na wajumbe kutoka takriban nchi 200 wanakongamana kwenye kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu Mabadiliko ya hali ya anga,ambalo limengoa nanga huko Glasgow,Scotland,leo Katika mkutano huu wa COP26, maswala kadha yatajadhiriwa hususan jinsi ya kupunguza utoaji gesi ya carbon kufikia mwaka 2030 na kunusuru dunia kutoa kwa adhari za mabadiliko ya hali ya anga. K ongamano hili litafanyika kwa majuma mawili,huku fursa ya kwanza ikitolewa kwa Shirika la utabiri wa hali ya anga duniani ili kutoa ripoti kuhusu hali ya anga ilivyo kufikia sasa.Lengo likiwa kutathmini viwango vya joto duniani kufikia mwaka huu na miaka ya awali. Zaidi ya hayo, ripoti imeandaliwa na itatolewa na wanasayansi wa hali ya anga. Hali ya anga imebadilika kwa kasi huku shughuli za wanadamu zikitolewa kama chanzo kuu cha mabadiliko hayo. Viwango vya juu zaidi vya joto, mafuriko na moto misituni inazidi kuongezeka,jambo ambalo linatia hofu. Mkutano huu una...