Jumatatu, 27 Februari 2012

Mzee Nelson Mandela apata matibabu

Aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini mzee Nelson Mandela aendelea kupata nafuu baada ya kutoka hospitalini , alikolazwa kutokana na maumivu ya tumbo ambaye yamekuwa yakimtatiza kwa muda mrefu.

Hapo awali, taarifa kutoka ofisi ya Rais Jacob Zuma ilisema Mzee Nelson Mandela alilazwa hospitalini na akawaomba  Waafrika Kusini kumuombea nafuu ya haraka.

Mzee Mandela, mwenye umri wa miaka 93 hajaonekana hadharani kwa muda mrefu sasa kufuatia kudorora kwa afya yake .

Wananchi wengi nchini Afrika Kusini walipokea habari za kulazwa kwake hospitalini kwa hofu na huzuni tele, lakini wakasema wanaendelea kumuombea apate afueni ya haraka.

Mbali na hayo,mzee Mandela aligunduliwa  kuugua saratani ya tezi dume,2001 na baada ya matibabu akapona, kwani iligunduliwa mapema.

Alikuwa Rais wa kwanza mweusi katika nchi hiyo kuanzia mwaka 1994 na kisha akaachia ngazi mwaka 1999.

Mandela anatambulika kote duniani kwa juhudi zake za kupambana na utawala wa kibaguzi wa Makaburu kwa muda mrefu na baadaye kuikomboa Afrika Kusini kutoka mikononi mwa wabaguzi hao wa rangi katika muongo wa tisini.


Pia sisi hapa nchini Kenya tunashukuru Mola kwa kumlinda mzee Mandela na pia tunamuombea ampate afueni.

Alhamisi, 23 Februari 2012

Njenga Karume aaga dunia

Former Kenyan Defense Minister NJenga Karume Dies Of Cancer: Sources
Marehemu Njenga Karume
Aliyekuwa waziri wa ulinzi na mbunge wa zamani wa Kiambaa, Njenga karume amefariki dunia.

Karume ameaga dunia katika hospitali ya Karen hapa Nairobi ,alipokuwa akipokea matibabu, baada ya kuugua saratani. Marehemu Karume amefariki akiwa na umri wa miaka 83.

Rais Mwai Kibaki ametoa salamu zake za rambi rambi kwa jamaa na marafiki wa Marehemu huku akisema amempoteza rafiki wa dhati.

Karume alikuwa kigogo wa siasa na alimuunga mkono rais Mwai Kibaki katika juhudi zake za kuimarisha siasa za chama cha Democratic party(DP).

Karume alikuwa mwanabiashara mashuhuri ambaye alikuwa na bidii kama za mchwa.Alijizatiti kuwa mmojawa  matajiri watajika hapa nchini,licha ya kuanzia chini sana.

Katika kitabu chake, alichoandika kuhusu maisha yake, Karume alisema vile alijitahidi kutoka uchomaji wa makaa hadi dhahabu.
Anatajwa pia kama aliyepigania uhuru, aliyehakikisha tamaduni zinahifadhiwa.

Alikuwa mbunge wa kiamba lakini 2007 alipoteza kiti chake, aliposhindwa na mbunge wa sasa mheshimiwa Stanley Githunguri.

Alikuwa pia mwanzilishi wa kundi la Gikuyu Embu Meru Association(GEMA) na mstahiki mzee wa jamii ya Gikuyu.

Wiki mbili kabla ya kifo chake uvumi ulienezwa kuwa Karume alikuwa amefariki.Kufuatia uvumi huo Rais Kibaki alimtembelea nyumbani kwake huku Cianda, Kiamba katika jimbo la Kiambu.

Mungu ailaze roho yake Karume pema peponi.




Hii ni aina ya saratani inayokumba tezi ya thyroid. Ikumbukwe kuwa tezi ya thyroid ipo sehemu ya mbele ya shingo ya mwanadamu ikiwa na sehemu mbili (lobes) moja kila upande wa shingo.
Visababishi na ukubwa tatizo
Saratani ya thyroid huwapata watu wa umri mbalimbali, kuanzia watoto mpaka watu wazima. Watu waliowahi kupigwa mionzi sehemu ya mbele ya shingo wapo katika hatari kubwa ya kupata aina hii ya saratani. Kadhalika watu wazima ambao waliwahi kupigwa mionzi kipindi cha utotoni nao pia wana hatari kubwa zaidi ya kupata saratani ya thyroid hata kama hawakuwahi kupata tatizo hilo wakati wanakua.
Tiba ya mionzi maeneo ya shingoni ilikuwa ikitumika sana zamani kwenye miaka ya 50 mpaka 60 kwa ajili ya matibabu ya uvimbe wa tezi ya thymus, mafindofindo (tonsils), au baadhi ya magonjwa ya ngozi. Hata hivyo ni nadra sana kwa tiba hii kutumika katika zama hizi.
Vihatarishi vingine vya saratani ya tezi ya thyroid ni pamoja na kuwepo kwa historia ya tatizo hili miongoni mwa wanafamilia na kuwa na goita iliyodumu muda mrefu bila kutibiwa.
Aina za saratani ya tezi ya thyroid
Kulingana na aina ya seli zinazounda tezi ya thyroid zinazoshambuliwa, saratani ya thyroid inaweza kugawanywa katika aina zifuatazo:
•    Aina inayojulikana kitaalamu kama papillary carcinoma. Hii ni aina  maarufu zaidi miongoni mwa watu wenye saratani ya tezi ya thyroid. Kwa kawaida, aina hii huwapata zaidi wanawake walio katika umri wa kuzaa. Aina hii husambaa taratibu sana na haina madhara sana kwa mgonjwa ikilinganishwa na aina nyingine za saratani ya tezi ya thyroid.
•    Aina nyingine ni ile inayofahamika kwa jina la follicular carcinoma. Aina hii hutokea katika asilimia karibu 10 ya watu wanaopata saratani ya thyroid. Follicular carncinoma huwa na tabia ya kupotea lakini pia huwa na uwezo  wa kumrudia mgonjwa na kisha kusambaa kwa kasi.
•    Aina ya tatu ni ile inayojulikana kama anaplastic carcinoma. Aina hii, japokuwa ni nadra sana kuonekana miongoni mwa wagonjwa wenye saratani ya thyroid, ndiyo aina ya  hatari zaidi miongoni mwa aina zote za saratani ya thyroid. Anaplastic carcinoma husambaa kwa kasi kubwa na haiwezi kutibika kwa kutumia tiba ya madini ya nuklia ya Iodine.
•    Aina nyingine huitwa medullary carcinoma. Hii ni aina ya saratani ya thyroid ambayo hutokea katika seli ambazo si za tezi ya thyroid lakini zipo ndani ya tezi hiyo (kuna baadhi ya seli ambazo si za tezi ya thyroid lakini zinapatikana na kuishi ndani ya tezi ya thyroid, mfano wa mgeni anayeishi katika nyumba isiyo yake). Aina hii huwapata zaidi wanafamilia na watafiti wameihusisha na mabadiliko ya kinasaba (genetic mutations), na kwa ujumla matibabu yake hutofautiana sana na yale ya aina nyingine za saratani ya thyroid.
Dalili
Dalili hutofautiana kulingana na aina ya saratani, ingawa kiujumla zaweza kujumuisha:
•    kikohozi
•    Shida wakati wa kumeza chakula, vinywaji hata mate
•    Kuvimba kwa tezi ya thyroid
•    Mabadiliko katika sauti, sauti kufifia au kuwa ya mikwaruzo
•    Uvimbe kwenye shingo
•    Tezi ya thyroid kuwa na nundu au vinundu
Vipimo na uchunguzi
Mgonjwa anayehisiwa kuwa na saratani ya thyroid hufanyiwa uchunguzi wa mwili kabla ya kufanyiwa vipimo kadhaa ili kujiridhisha kuwa ni kweli ana tatizo la saratani ya thyroid. Uchunguzi wa mwili unaweza kuonesha uwepo wa nundu au uvimbe katika thyroid na/ kuvimba kwa tezi za mitoki katika shingo.
Vipimo ni pamoja na:
•    Ultrasound ya tezi ya thyroid
•    Kukata sehemu ya thyroid na kukichunguza kimaabara (thyroid biopsy)
•    Picha ya utendaji kazi wa tezi ya thyroid (thyroid scan)
•    Uchunguzi wa sehemu ya ndani ya koo (laryngoscopy)
•    Kupima damu ili kuchunguza kiwango cha homoni ya calcitonin. Iwapo kiwango kitakuwa juu kuliko kawaida, hii yaweza kuashiria uwepo wa medullary carcinoma.
•    Kupima damu ili kuchunguza kiwango cha viasili vya thyroglobulin ambavyo vywaweza kuashiria uwepo wa saratani aina ya papillary carcinoma au follicular carcinoma.
•    Kupima damu ili kuchunguza kiwango cha homoni za thyroid za T3, T4 na TSH.
Matibabu
Matibabu hutegemea sana aina ya saratani, ingawa upasuaji wa tezi ya thyroid ndiyo aina ya tiba inayoongoza. Wakati wa upasuji, kwa kawaida tezi yote huondolewa, na iwapo daktari atahisi kuwa hata tezi za mitoki zilizo karibu na thyroid nazo pia zimeathirika pia huondolewa.
Aidha mgonjwa anaweza pia kupatiwa tiba ya mionzi ambayo hutolewa kwa njia ya kupigwa mionzi ya moja kwa moja (external beam radiation) au kwa kutumia (kunywa) vidonge vya madini ya Iodine vyenye nguvu ya nyuklia yaani radioactive iodine. Njia hii inaweza kufanyika ikiambatana pia na upasuaji au bila upasuaji.
Baada ya matibabu, mgonjwa anapaswa kuendelea kutumia dawa maalum za kumrejeshea homoni za thyroid ili kurudisha kile alichopoteza baada ya kuondolewa kwa tezi. Kwa kawaida dozi inayotolewa huwa kubwa kuliko ile inayohitajika mwilini ili kusaidia saratani isijirudie tena.
Iwapo upasuaji au mionzi haujasaidia kuondoa kansa, na kwamba saratani inaendelea kusamabaa sehemu nyingine za mwili, mgonjwa anaweza kuanishiwa dawa za kutibu saratani (chemotherapy) ingawa nayo inaweza ikawa na manufaa kwa baadhi ya wagonjwa tu na si wagonjwa wote.
Nini cha kutarajia
Saratani aina ya Anaplastic carcinoma ina matokeo mabaya zaidi kuliko aina zote zilizobaki, na mara nyingi mgonjwa hufariki hata baada ya matibabu ya uhakika ya muda mrefu. Follicular carcinomas pamoja na kuwa na tabia ya kusambaa kwa kasi kwenye maeneo mengine ya mwili huwa na matokeo mazuri ikitibiwa. Matokeo ya wagonjwa wenye aina ya medullary carcinoma yanatofautiana kati ya mgonjwa na mgonjwa, ambapo wanawake wenye umri chini ya miaka 40 wameonekana kuwa na matokeo mazuri zaidi baada ya tiba kuliko walio na zaidi ya umri huo. Aidha wagonjwa wengi wenye Papillary carcinomas hupona kabisa na kuendelea na maisha yao ya kawaida.
Jambo la kukumbuka ni kuwa, mara baada ya tiba, mgonjwa anapaswa kuendelea kutumia vidonge vya kurejesha homoni za thyroid kila siku za maisha yake.
Madhara ya saratani ya thyroid
Madhara ya saratani ya thyroid ni pamoja na madhara katika sanduku la sauti kabla ya upasuaji, na sauti ya mikwaruzo baada ya upasuaji, kupungua kwa kiwango cha madini ya calcium mwilini iwapo tezi ya parathyroid ambayo ipo juu kidogo ya thyroid itaodolewa kwa bahati mbaya wakati wa upasuaji, na kusambaa kwa kansa katika sehemu nyingine za mwili kama vile mifupa, au mapafu.
Kinga
Mpaka sasa hakuna kinga rasmi ya ugonjwa huu. Hata hivyo, ni vizuri jamii ikawa makini na mionzi isiyohitajika sehemu za mbele ya shingo. Aidha wale wenye historia ya tatizo hili katika familia zao ni vema wakamuona daktari kwa ajili ya uchunguzi kabla tatizo halijajitokeza, au kuwa kubwa.


Marehemu Michuki aombolezwa



Marehemu John Michuki
 Wakenya wa tambaka mbalimbali waendelea kuomboleza kifo cha aliyekuwa waziri wa mazingira John Njoroge Michuki aliyefariki dunia jumanne,kwa mstuka wa moyo,  katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Aga Khan.

Akizaliwa 1932 katika kitongoji cha Jimbo la Kagema katika wilaya ya Muranga.
Alipata masomo yake ya upili katika shule ya Mangu pamoja na rafikiye wa dhati  rais Mwai Kibaki.

Aliendelea na masomo yake katika chuo cha Worcester,Oxford huko Uingereza.
Wengi wamemtaja michuki kama kiongozi  mchapa  kazi , aliyedumisha nidhamu ya hali ya juu kazini na aliyejitolea kwa kila alilofanya.

Rais Mwai Kibaki ambaye ni rafikiye marehemu alisema kuwa Michuki alikuwa mwanasiasa hodari,aliyetekeleza kazi yake kwa uadilifu.Pia mwana biashara stadi.
Kulingana na mhariri wa habari wa kujitengemea Onesmus Kilonzo Michuki atakubukwa kwa kulainisha sekta ya matatu,na uhifadhi wa mto Nairobi miongoni mwa mengine

“kila ofisi aliohudumia ilipata ufanisi mkubwa.Wengi watamkumbuka milele kwa ukakamavu wake wa utenda kazi”,alisema Kilonzo.

Wabunge jana wariahirisha shughuli za mbunge kuomboleza kifo cha mwenda zake Michuki.Kila aliye nena alimumiminia sifa Michuki na kusema kuwa ameacha pengo ambalo kwa hakika halitazibika.

Mbunge wa Gichungu Martha Karua ambaye pia ni mgombeaji wa kiti cha urais alisema endapo alitofautiana kisiasa na marehemu, Michuki alikuwa kiongozi mwenye hekima na ukakamavu wa hali ya juu.

Mbunge Amina Abdalla pia alimtaja kama baba aliyewataka vijana watie bidii katika lolote wafanyalo.

Wengine waliomsifu michuki ni pamoja na wakuu wa shirika la mazingira duniani UNEP waliosema kuwa alionyesha ubunifu na makini katika maswala ya mazingira.

Baadaye jioni  makamu wa rais kalonzo musyoka ,spika wa mbunge Kenneth Marende na baadhi ya wambunge walitembelea familia ya michuki nyumbani kwake Ridgeways.

Rais Kibaki  ametatangaza kuwa kupeperushwa kwa bendera nusu mlingoti kwa heshima ya mwenda zake Michuki.

Michuki atazikwa siku ya jumanne huko Kagema.

Mungu amlaze mahali pema peponi.


Jumatatu, 20 Februari 2012

WHO yasema depo provera ni salama



Shirika la Afya Duniani ( WHO) limeondolea lawama shindano ya Depo Provera kuwa inachangia maambukizi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU).

Shirika hili (WHO) linahakikishia  wanawake wanaotunia aina ya uzazi wa mpango wa homoni kuwa hakuna hatari ya kutumia aina hii, kama ilivyo daiwa hapo wali.

Hata hivyo (WHO) imeonya  kuwa  ni aina moja pekee ya uzazi wa mpango inayozuia maambukizi ya Virusi  Vya Ukimwi - kondomu au mpira.

Huku likisisitiza kuwa ni muhimu kwa wale wako kwenye hatari ya kuambukizwa Virusi Vya Ukimwi kuchukua tahadhali.

Zaidi ya hayo, Shirika la Afya Duniani utafiti unafanywa kwa nia ya kuhakikisha malengo ya milenia ya afya imefikiwa.
Uvumbuzi kuwa utumiaji dawa ya upangaji uzazi ya homoni ijulikanayo kama Devo Provera unachangia ongezeko la maabukuzi ya ugonjwa hatari wa ukimwi, miezi michache iliyopita, uliwaacha wanawake wengi na hofu na husuni tele.
Inakadiriwa kuwa takribani millioni 12 ya wanawake wenye umri wa kati ya  miaka 15 na 49 katika Afrika kusini na Jangwa la Sahara wanatumia homoni za kuzuia mimba(Depo provera).

Takwimu hizi zilitolewa na shirika moja la afya la Marekani lililofanya utafitia uliochapishwa  na jarida la The Lancet.

Shirika hili la afya, lilitoa tahadhali kuwa  akina mama wanaotumia aina ya uzazi  upangaji wa homoni(Depo Provera) wako  hatarini ya kuambukizwa au kuwaambukiza waume wao Virusi Vya Ukimwi ,kuliko wale wasiotumia aina hii.

Kufuatia utafiti huu,Shirika la Afya Duniani (WHO) liliitisha kikao cha dharula Januari mwaka huu (2012) ili kutadhimini iwapo ushahidi huu unatosha kuwashauri wanawake kuachana na aina hii ya mpango wa uzazi ili kukomesha maambukizi zaidi.

Kutokana na matokeo haya, ni vyema kwa yeyote anayetumia aina yeyote ile ya mpango wa uzazi kufahamu kuwa, endapo kundomu haitumiwi panapo hatari ya maambukizi, basi yule mwanamke au mwanaume atakuwa akihatarisha maisha yake.
Kuzuia ni bora kuliko kuponya.

Ni jukumu ya kila mtu kuhakikisha analinda afya yake kutokana na mikasa ya kujitakia, kwani mkasa wa kujitakia hauna kilio.






Ijumaa, 10 Februari 2012

Saratani ya tezi kibofu cha mkojo (Prostate)

 

Saratani ya tezi kibofu ni ugonjwa ambao  huwa kati ya wanaume.kama aina nyingine za saratani, inapogunduliwa mapema inakuwa ni rahisi kutibiwa. Zaidi ya hayo, walio  hatarini ya kuambukizwa Ugonjwa huu ni  wanaume walio na umri wa miaka 55 na zaidi.

Hivi majuzi, ugonjwa wa saratani umetia wengi kiwewe.Siku baada ya siku kuna habari kuwa mtu fulani ana ugonjwa wa saratani.Waume kwa wanawake,vijana  kwa watoto wote wako hatarini ya kuabukizwa ugonjwa huu.

Watafiti bado hawajapata uvubuzi ni nini haswa inayo sababisha ugonjwa huu hatari.

Hata hivyo inakisiwa kuwa  mazingira tunayoishi, kwa njia moja ua nyingine yanachangia kuwepo kwa maradhi haya.

Hapa nchini Kenya waziri wa  afya ya umma Mheshimiwa Beth Mugo alitangaza kuwa amegunduliwa kuugua saratani ya matiti na kwa sasa anaendelea na matibabu huko Marekani.

Waziri Mwenzake, Prof. Anyang Nyongo pia aligunduliwa kuugua saratani ya tezi kibofu.Kwa bahati nzuri, iligunduliwa mapema na baada ya matibabu ya muda, madaktari walimhakikishia  kuwa amepona.

Pia mwanahabari mashuhuri Jerry Okungu ana saratabni ya tezi kibofu.Amekuwa akikabiriana na ugonjwa huu kwa muda sasa.Afueni ni kuwa haja kata tamaa na ameanzisha wakfu wa saratani ili kuwaelimisha na kuwasaidia wale wasioweza kugharamia matibabu.

Matibabu ya saratani huwa ghali mno,hivyo basi wale wanaougua wanakubwa na matatizo ya kutafuta matibabu,hii huchangia kuzorota kwa afya na hata maafa.

Ugonjwa huu ambao huambukiza chini ya kibofu cha mikojo,huwapata wanaume weusi kwa asili mia kubwa ikilinganishwa na wale wa asili zingine ulimwenguni.

Ili kutambua kuwa mtu anaugua saratani ta tezi kitofu, wataalamu wa afya hufanya  uchunguzi  kwa kutumia kemikali ya “Prostate specific antigen” au PSA katika damu ya mgonjwa, ikiwa kuna idadi ya juu ya PSA , waweza kuwa na ugonjwa huu.

·       Wanaume wengine wamo hatarini kupata saratani ya mamalia dume:

·      Wanaume ambao wamekuwa na jamaa kama baba au kaka ambao   washauguwa ugonjwa huu.

·         Kula vyakula vingi vya mafuta, nyama nyekundu, siagi na maziwa. 

Dalili ya saratani ya mamalia dume:

·          Kukojoakojoa kila mara hasa wakati wa siku.

·          Kuwa na shida za kuanza kukojoa au kusitiri mikojo.

·          Kukojoa kwa matone matone.

·          Kuhisi uchungu au moto unapokojoa

·          Kuhisi uchungu unapomwaga manii.

·          Kukojoa mikojo iliyochanganyika na damu.

·          Maumivu ya kila mara hasa sehemu za mgongo,nyonga au mapajani sehemu za juu.