Ijumaa, 6 Desemba 2013



Mandela aaga dunia akiwa na umri wa miaka 95


  • Nelson Mandela pamoja na mkewe, Winnie, wakiwapungia mkono watu walojitokeza kumpokea alipoachiwa huru kutoka jela ya Victor Verster hapo Februari 11, 1990. 

Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ametangaza Ijumaa usiku kwamba rais wa zamani mpinzani mkuu wa ubaguzi wa rangi Madiba Nelson Mandela amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu. Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ametangaza Ijumaa usiku kwamba rais wa zamani mpinzani mkuu wa ubaguzi wa rangi Madiba Nelson Mandela amefariki baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Akilihutubia taifa Rais Zuma alisema "Taifa letu limempoteza mwana wake mkuu shujaa. watu wetu wamempoteza baba yao"
Mandela alikuwa rais wa Kwanza muafrika kuchukua madaraka kutoka kwa utawala wa ubaguzi wa rangi kutoka kwa wazungu walowachache 1994. Kwa wengi alikua shujaa, mtu shupavu na mwenye mtizamo.

Mara kwa mara alikuwa mnyenyekevu, mchangamfu, muaminifu na mtu ambae aliwajali wananchi wote.
Wasifu wa Mandela

Mwaka 1962, Madiba jina lake maarufu huko Afrika Kusini alikamtwa na kushtakiwa kwa tuhuma za kufanya vitendo vya kutaka kuihujumu serikali. Hata hivyo alijitetea akisema hivyo vilikuwa vitendo vya kuwakomboa waafrika walowengi. Miaka miwili baadae alihukumiwa kifungo cha maisha katika kiswa cha Robben kwenye pwani ya mji wa magharibi wa Cape Town.

Mandela aliachiwa huru miaka 27 badae, ikiwa mwaka 1990 pale serikali ya wazungu wachache iliyokua inaongozwa na Rais Frederik De Klerk kuhalalisha vyama vyote vya kisiasa na kuwafungua wafungwa wote wa kisiasa.

Utawala wa mpito ulienddelea na majadiliano ya kutayarisha katiba na utawala wa kidemokrasia ulianza ukiongozwa na Mandela na De Klerk. Uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vyote na watu wa kabila zote ulifanyika 1994 na Mandela kuchaguliwa akiwa na umri wa miaka 74.

Mandela na mkewe Winnie walikuwa pamoja baada ya kuachiliwa huru kutoka gereza la Robben Island, lakini hai8kuchukua muda wakaachana. Na katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake alipotimiza miaka 80 alimuoa Graca machel, mjane wa rais wa zamani wa Msumbiji Samora Machel.

Alibaki madarakani kwa mhula mmoja wa miaka mitano, na kuanza kampeni chungu nzima moja wapo ikiwa ni kutetea haki za watoto na kupambana na ugonjwa wa Ukimwi. Akiwa madarakani alikosolewa kwa kutokubali kuchukua hatua za nguvu kupambana na janga hilo.

Miaka miwili baada ya kuondoka madarakani mtoto wake wa kiume alifariki kutokana na ukimwi na hapo ndipo aliongeza juhudi zake za kupambana na ugonjwa huo.

Akiwa na umri wa miaka 85 hapo mwaka 1999 Mandela alitangaza kwamba anastahafu kabisa kutoka kazi za umaa lakini aliendelea kufanya kazi kutetea haki za watoto.

Mnamo maisha yake yote alipokea mamia ya tunzo lakini tunzo kuu ni ile ya amani ya Nobel ya 1993aliyopata pamoja na hasimu wake rafiki yake Bw De Klerk. 
VOA

Alhamisi, 5 Desemba 2013

Masuala ya Jamii

Ripoti ya Ufaransa: Arafat hakufa kwa sumu

Uchunguzi uliofanywa na wanasayansi wa Ufaransa kuhusu kifo cha kiongozi wa zamani wa Palestina, Yasser Arafat, umeonyesha kuwa kiongozi huyo hakufa kutokana na sumu ya Polonium, bali alikufa kifo cha kawaida.
Marehemu Yasser Arafat Marehemu Yasser Arafat
Kwa mujibu wa ripoti ya uchunguzi wa wanasayansi hao, vipimo vimeonyesha kuwa Arafat alikufa kutokana na uzee baada ya kupata maambukizi na sio kutokana na sumu ya polonium, ingawa wamesema kulikuwa na ishara za plotunium.
Matokeo hayo yanatofautiana na ripoti iliyotolewa awali na maabara moja ya Uswisi, iliyoeleza kuwa Arafat alikufa kutokana na kiwango kikubwa cha sumu ya polonium, baada ya kuigundua sumu hiyo kwenye nguo zake.
Ripoti hiyo ya Ufaransa imepingwa vikali na mke wa Arafat, Suha Arafat, ambaye amesema kifo cha mumewe kilikuwa ni mauaji ya kisiasa yaliyofanywa na mtu wake wa karibu. Akizungumza mjini Paris, Suha amesema ameshangazwa na taarifa zinazokinzana kutoka kwa waatalamu wa Ulaya.
Ripoti hiyo iliyokabidhiwa kwa Suha, haitachapishwa, lakini ofisi ya mwendesha mashtaka wa serikali imesema uchunguzi uliokamilika unaoonyesha kuwa Arafat hakuuawa kwa sumu ya polonium.
Arafat, aliyesaini makubaliano ya mjini Oslo ya mwaka 1993 na Israel, alifariki Novemba mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 75, katika hospitali moja nchini Ufaransa.
Kifo chake kilitokea wiki nne alipougua baada ya kula chakula na hivyo kusababisha kutapika na kuumwa tumbo. Taarifa za kitabibu zilionyesha kuwa alikufa kutokana na kutokwa damu katika ubongo, lakini hakukuwa na maelezo ya nini kilisababisha hali hiyo.
Palestina yapuuzia uchunguzi wa Ufaransa
Sumu ya Polonium iliyomuua jasusi wa Kirusi, Alexander Litwinenko. Sumu ya Polonium iliyomuua jasusi wa Kirusi, Alexander Litwinenko.
Afisa mwandamizi wa Palestina, Wasel Abu Yousef, ameipuuza ripoti hiyo ya Ufaransa akisema kuwa iko kisiasa zaidi na iko kinyume na ushahidi unaothibitisha kuwa Arafat aliuawa kwa kupewa sumu.
Wapalestina wengi wanaamini kuwa Israel inahusika na kifo cha kiongozi wao, tuhuma ambazo Israel imezikanusha.
Mkuu wa kamati ya Palestina inayochunguza kifo cha Arafat, Tawfik Tirawi amesisitiza kuwa Israel inahusika na awali alisema atataja majina ya watu wanaoaminika kuhusika na kifo cha kiongozi huyo.
Hata hivyo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Israel, amesema kuwa ripoti ya matokeo ya Ufaransa si ya kushangaza na kuelezea matumaini yake kwamba sasa Arafat atapumzika kwa amani.
Mwaka uliopita, mjane wa Arafat aliitaka serikali ya Ufaransa ifanye uchunguzi wa kifo cha mumewe, baada ya kituo cha televisheni cha Al Jazeera kuripoti kwamba nguo za Arafat zilikutwa na sumu ya polonium.
Waendesha mashitaka wa Ufaransa walianzisha uchunguzi na hatimaye wataalamu wa kupekuwa ushahidi kutoka Uswisi, Urusi na Ufaransa, walichukua sampuli za mabaki ya mwili wa Arafat, baada ya kufukuliwa mwaka 2012.

DW.DE


Ijumaa, 22 Novemba 2013

Mpango mpya kuboresha huduma za uzazi wa kupanga baada ya kujifungua mimba: WHO



Unyonyeshaji mtoto baada ya kujifungua ni mojawapo ya njia za uzazi wa mpango- WHO
Shirika la Afya Duniani, WHO, limezindua mpango mpya wa kuboresha upatikanaji wa huduma za uzazi wa kupanga kwa akina mama katika miezi 12 ya kwanza baada ya kujifungua, ambao unawalenga wahudumu wa afya na watunga sera. Kwa mujibu wa WHO, mimba zinazokaribiana sana au zisizotarajiwa ni tishio la kiafya kwa mama na mtoto, na kwamba kuweka pengo la angaa miaka miwili kabla ya mimba nyingine kunaweza kuepusha asilimia 10 ya vifo vya utotoni na takriban kuepusha kifo kimoja kati ya vitano miongoni mwa watoto wenye umri kati ya mwaka mmoja hadi minne. Mpango huo ambao umezinduliwa katika kongamano la kimataifa kuhusu uzazi wa kupanga mjini Addis Ababa, Ethiopia, unanuia kuitikia mahitaji kwa ngazi zote za huduma za afya, ili kuongeza upatikanaji wa huduma za uzazi wa mpango kwa akina mama mara tu baada ya kujifungua. Takwimu kutoka nchi 27 zinazoendelea zinaonyesha kuwa asilimia 95 ya wanawake wanataka kujiepusha na mimba kwa angaa miaka miwili baada ya kujifungua, lakini asilimia 65 kati yao-Redio ya UM

Jumatano, 16 Oktoba 2013

 

Saratani tezi

Huku ukiwa mwezi wa kupambana na janga la ugonjwa wa saratani,watu wengi hawapendi  kwenda hospitalini kwa uchunguzi,huku wakihofia kugunduliwa na maradhi ya saratani.
Hii ni baadhi ya sababu zinazopelekea ongezeko la saratani nchini kenya na kanda la afrika kwa jumla.
Inakisiwa kuwa zaidi ya watu elfu moja(1,000)  huugua saratani huku zaidi ya  850 wakifariki kila mwaka.
Takwimu pia zinaonyesha idadi ya saratani ya tezi kibofu inaongezeka marudufu.

Saratani ya tezi kibofu ni ugonjwa ambao  huwa kati ya wanaume.kama aina nyingine za saratani, inapogunduliwa mapema inakuwa ni rahisi kutibiwa. Zaidi ya hayo, walio  hatarini ya kuambukizwa Ugonjwa huu ni  wanaume walio na umri wa miaka 55 na zaidi.

 Kulingana na watalaamu wa afya watu wengi hutafuta tiba wakati ugojwa umeenea zaidi.

Hivi majuzi, ugonjwa wa saratani umetia wengi kiwewe.Siku baada ya siku kuna habari kuwa mtu fulani ana ugonjwa wa saratani.Waume kwa wanawake,vijana  kwa watoto wote wako hatarini ya kuabukizwa ugonjwa huu.

Watafiti bado hawajapata uvubuzi ni nini haswa inayo sababisha ugonjwa huu hatari.

Hata hivyo inakisiwa kuwa  mazingira tunayoishi, kwa njia moja ua nyingine yanachangia kuwepo kwa maradhi haya.

Waziri Mwenzake, Prof. Anyang Nyongo pia aligunduliwa kuugua saratani ya tezi kibofu.Kwa bahati nzuri, iligunduliwa mapema na baada ya matibabu ya muda, madaktari walimhakikishia  kuwa amepona.

Pia mwanahabari mashuhuri Jerry Okungu ana saratabni ya tezi kibofu.Amekuwa akikabiriana na ugonjwa huu kwa muda sasa.Afueni ni kuwa haja kata tamaa na ameanzisha wakfu wa saratani ili kuwaelimisha na kuwasaidia wale wasioweza kugharamia matibabu.

 

Matibabu ya saratani huwa ghali mno,hivyo basi wale wanaougua wanakubwa na matatizo ya kutafuta matibabu,hii huchangia kuzorota kwa afya na hata maafa.

Ugonjwa huu ambao huambukiza chini ya kibofu cha mikojo,huwapata wanaume weusi kwa asili mia kubwa ikilinganishwa na wale wa asili zingine ulimwenguni.

Ili kutambua kuwa mtu anaugua saratani ta tezi kitofu, wataalamu wa afya hufanya  uchunguzi  kwa kutumia kemikali ya “Prostate specific antigen” au PSA katika damu ya mgonjwa, ikiwa kuna idadi ya juu ya PSA , waweza kuwa na ugonjwa huu.

·       Wanaume wengine wamo hatarini kupata saratani ya mamalia dume:

·      Wanaume ambao wamekuwa na jamaa kama baba au kaka ambao   washauguwa ugonjwa huu.

·         Kula vyakula vingi vya mafuta, nyama nyekundu, siagi na maziwa. 

Dalili ya saratani ya mamalia dume:

·          Kukojoakojoa kila mara hasa wakati wa siku.

·          Kuwa na shida za kuanza kukojoa au kusitiri mikojo.

·          Kukojoa kwa matone matone.

·          Kuhisi uchungu au moto unapokojoa

·          Kuhisi uchungu unapomwaga manii.

·          Kukojoa mikojo iliyochanganyika na damu. 

 

Alhamisi, 10 Oktoba 2013


 The 2013 International Conference on Family Planning: 


Family Planning






Katika juhudi za kuboresha afya ya akina mama,shirika la mpango uzazi duniani litafanya Mkutano wa Mpango uzazi  nchini Ethiopia mwezi wa Novemba mwaka huu.










Mkutano huu unafanyika huku karibu watu millioni 900 kote duniani wakikumbatia uzazi wa mpango.

Hata hivyo, sio wote wanaoweza kufanya uzazi wa mpango wakati wanapotaka kufuatia changamoto kadha wa kadha.

Mkutano huu utawajumuisha watafiti wa afya,madaktari na wadau wengine katika sekta ya afya.


Inaaminika kuwa wazazi wengi ambao wangependa kupanga uzazi wanasubuka sana.Hata kabla wapate huduma hiyo muhimu wanagundua kuwa ni wajawazito.Idadi ya wanandoa walio kwenye hali hii ni zaidi ya millioni 215 kote duniani.

 Uzazi wa mpango unawezesha wanandoa kufanya maamuzi ya uzazi na ni moja ya njia ya gharama nafuu kwa ajili ya kuboresha afya  ya familia. 
Kilingana na takwimu za shirika laThe Bill & Melinda Gates  idadi ya 287,000 ya wanawake hufariki kila mwaka katika hali ya ujauzito.
 




Jumanne, 8 Oktoba 2013





 


Mwezi wa Oktober ni mwezi wa kuelimisha umma jinsi ya kupambana na ugonjwa hatari wa saratani hususan ile ya matiti.
Hata hivyo juhudu za kupambana na saratani haziridhishi kutokana na ukosefu wa vifaa vya kugundua na kuutibu.



Baadhi ya wakenya wamelalamika kuwa vifaa duni katika hospitali za umma kunachangia ongezeko la idadi ya wanaofariki kila siku kutokana na saratani.

Pia,Upungufu wa watalaamu wa saratani huku baadhi yao kukikimbilia hospitali za binafsi ambapo wanapata mishahara yakulidhisha.

Hivyo basi ni jukumu la serikali kuhakikisha kuna vifaa vya kisasa.Na kuongeza mishahara kwa watalaamu wa afya.
Kwa sasa,idadi kubwa ya wakenya hutafuta matibabu ya saratani nchini India ambapo ghalama ya matibabu ni nafuu.

Hata hivyo, sio kila mtu au jamaa inaweza kugharamia matibabu ya saratani India.
Ni jukumu ya serikali kuhakikisha kuwa wanachi hawafariki kutokana na ugonjwa huu kwa sababu ya gharama au musongamano wa wangonjwa unaopelekewa na upungufu wa vifaa vya matibabu.

Mikakati muhimu na ya dharura inahitajika ili kupungunga au kukambilaiana nahali hii ya kuhuzunisha.
Ugonjwa huu umekuwa tishio nchini kenya na pia nchi zinachoendelea.
Hata hivyo,kuna sababu ya kutokufaa moyo ,kwani ugonjwa unapogunduliwa mapema,mgonjwa anaweza akapona.

Baadhi ya dalili ni kama vile;
-Kuwepo kwa uvimbe kwenye sehemu za kwapa
-Sehemu ya titi kuingia ndani 
-Mabadiliko kwenye chuchu
-kidonda kwenye chuchu
-chuchu hutokwa damu au maji yasiyo ya kawaida
 -ngozi kuwa na rangi nyekundu.

Jumatatu, 27 Mei 2013

midwife



Wakunga na uzazi
Usimtukane  mkunga na uzazi ungalipo.Hii ni methali inayotuonya tusiwadharau au kuwatukana watu tunaowahitaji kwa jambo moja au nyingine, maishani

Kwa muda mrefu,wakunga wamekuwa wakitoa huduma zao kwa kina mama wajawazito hivyo basi wanaheshimika sana katika jamii.



 
Wiki iliyopita ilikuwa ni wiki muhimu sana kwani umoja wa mataifa ulitenda siku ya kuadhimisha Fistula  na pia mkutano wa wakunga duniani unaofanyika Kuala lumpur
Hii ni dhahiri kuwa afya ya uzazi inapewa kipao mbele duniani.
Wakati wa kujifungua kwa mwanamke, anakuwa kwenye hatari zaidi.
Wengi huvuja damu hadi kufa, wengine hupangi na tundu katika sehemu zao za uzazi-fistula.Pia anaweza akampoteza mwanawe katika hali ile ya kujifungua.

Ni kwa sababu hii akina mama wanahimizwa kuhudhuria vituo vya afya kwa uchunguzi na mafunzo ya kiafya.
Kulingana na taarifa za Umoja wa Mataifa,Wakunga wamechukua wajibu mkubwa katika jitihada za kupunguza hatari zinaowakumba wanawake wanapojifungua. Wakiwa na ujuzi wa juu, wakunga sasa wanaweza kukubiliana na  hatari zinaowakumba akina mama na wana wajibu mkubwa wa kuyaweka maisha  ya mama kuwa salama kote duniani.

Wakunga huwauguza akina mama kabla na baada ya kujifungua, wanalinda afya za watoto wanaozaliwa , wanatoa ushauri kuhusu upangaji uzazi, wanazuia maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto na wanafahamu wakati wa kuitisha huduma za dharura.
 
Inakadiriwa kuwa wakunga walio na mafunzo na wanaopata msaada wanaweza kuokoa  maisha ya zaidi ya wanawake 200,000 kila mwaka na mara kumi zaidi ya watoto kiasi hicho.
Washiriki katika kongamano na kuala lumpa wanasema kuna haja ya kuongeza idadi ya wakunga duniani ilikuepuka maafa yanayotokea wakati wakujifungua.

Pia hamazisho kwa akina mama ni muhimu;jambo ambalo mataifa yanayositawi na pia yaliostawi yanalitilia mkazo.
Ingawa pia wakunga wa jadi wanaheshimiwa kwa huduma zao, mara kwa mara hawana vifaa maalum endapo mama atashindwa kujifungua kwa njia ya kawaida.Hivyo basi wanahitaji kuelimishwa jinzi ya kukambiliana na hali za dharula.



Gharama za matibabu na umbali wa vituo vya afya ni changamoto ambalo pia ninastahili kushughulikiwa kwa haraka na serikali husika.

Endapo malengo yamilenia ya afya ya uzazi itaafikiwa basi ni sharti wahudumu wa afya washirikishwe .