saratani ya shingo ya uzazi (Cervical cancer)
Huku dunia ikiendelea kuadhimisha mwezi wa saratani duniani,idadi ya wanawake wanaoendelea kufariki kutokana na saratani ya shingo ya uzazi inazidi kuongezeka.
Aina hii ya saratani inasababisha vifo vya wanawake wengi nchi Kenya na duniani kwa ujumla.
katika shughuli zangu za kutafuta habari kuhusu ugonjwa wa saratani,nilipata fursa ya kuwahoji baadhi ya akina mama waadhiriwa na pia waliopona baada ya muda mrefu wa matibabu.
Mama Muthoni Kimani anasema alipona kutokana na ugonjwa huu kugunduliwa mapema,ijapokuwa aina ya matibabu na pia gharama ni ghali mno.
Wetende Ruth anasema kuwa angali anapokea matibabu na hakika ana imani atapoka.Jambo la muhimu ni kujipa moyo,anadokea watende.
"kabla
madaktari kugundua maradhi niliyokuwa nikiugua, nilikuwa nina maumivu
sana.Pia nilikuwa napata hedhi kila wakati,lakini si kufahamu kwamba
nilikuwa tayari naugua saratani ya shingo ya uzazi.
Kwa bahati nzuri.watalamu wa afya walitambua ni saratani ya shingo ya uzazi na papo hapo alianza matibabu".
Kwa sasa amepona na anatowa wito kwa aki mama wenzake wajipimishe mapema ili kuepana na hatari au tishio la ugonjwa huu.
Kulingana
na tarifaa za WHO ugonjwa huu unasabambishwa na virusi viitwavyo Human
Papiloma (HPV) ambavyo dalili zake huanza kuonekana miaka kumi baada ya
mgonjwa kuvipata.
Inakisiwa
kuwa idadi ya wanaougua ugonjwa huu unaongezeka kasi zaidi nchini
Kenya.Huku asilimia 35 wanawake wakihofiwa kuwa na virusi ya Human
Papilloma.Virusi hivi huambukizwa wakati wa kujamiana au kufanya ngono
ambapo mwanamke na mwanaume huambukizana virusi hivi.
Dalili
za ugonjwa huu,ni pamoja na kutokwa na damu ukeni wakati wa tendo la
ndoa, kuvuja damu hata baada ya hedhi,kuwa na maumivu wakati wa kufanya
ngono na pia kutoa harufu mbaya.
Mwaka
wa 2007,serikali ya Kenya ilianzisha mpango wa wanawake kujipimisha
ilikutambua mapema endapo wanaugua ugonjwa huu.Pia akina mama
wanashauriwa kupima kila mwaka, kwa kuwa wengi hupatwa na viashiria vya
saratani hii bila wao kutambua.
Kwa
kuwa kila mwanamke ambaye ameshiriki ngono yuko hatarini ya kupata na
ugonjwa huu.Serikali imetoa rai kwa kila mwanamke ambaye hana ugonjwa wa
saratani ya uzazi kupata chanjo inayopatikana katika vituo vya afya
nchini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni