The 2013 International Conference on Family Planning:
Katika juhudi za kuboresha afya ya akina mama,shirika la mpango uzazi duniani litafanya Mkutano wa Mpango uzazi nchini Ethiopia mwezi wa Novemba mwaka huu.
Mkutano huu unafanyika huku karibu watu millioni 900 kote duniani wakikumbatia uzazi wa mpango.
Hata hivyo, sio wote wanaoweza kufanya uzazi wa mpango wakati wanapotaka kufuatia changamoto kadha wa kadha.
Mkutano huu utawajumuisha watafiti wa afya,madaktari na wadau wengine katika sekta ya afya.
Inaaminika
kuwa wazazi wengi ambao wangependa kupanga uzazi wanasubuka sana.Hata
kabla wapate huduma hiyo muhimu wanagundua kuwa ni wajawazito.Idadi ya
wanandoa walio kwenye hali hii ni zaidi ya millioni 215 kote duniani.
Uzazi wa mpango unawezesha wanandoa kufanya maamuzi ya uzazi na ni moja ya njia ya gharama nafuu kwa ajili ya kuboresha afya ya familia.
Uzazi wa mpango unawezesha wanandoa kufanya maamuzi ya uzazi na ni moja ya njia ya gharama nafuu kwa ajili ya kuboresha afya ya familia.
Kilingana na takwimu za shirika laThe Bill & Melinda Gates idadi ya 287,000 ya wanawake hufariki kila mwaka katika hali ya ujauzito.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni