jambo la kutosisimuka kwa kimapenzi uwa ni jambo ambalo halizungumziwi kila mahali kwani akina mama wengi wanaliona la aibu.
Lakini wataalamu wa maswalaFlibanserin
Tembe ya kusisimua mapenzi
Wanawake kupungukiwa na nguvu na
hamu ya kufanya mapenzi imek la
afya ya akina mama wanaliona swala la kawaida ambalo linaweza kurekebishwa kwa
matibabu.
Lakini habari njema ni kuwa vidonge
vya kuwaimarishia wanawake hamu au hisia za kitendo cha ngono imeidhinishwa.Hii
ni afueni ambayo itaondoa aibu au kufujika kwa ndoa kutokana na kutoridhisha waume
wao.
Wataalamu wa afya wanasisitisha
kuwa kuna tofauti ya tembe hizi na zile za kiume za Viagra .
Shirika moja la Amerika la
kuidhinisha na kusimamia dawa liliidhinisha tembe za Flibanserin kutumiwa
kusisimua akina mama kimapenzi baada ya kufanya utafiti na kupata kuwa tembe
hizi ni salama.
Ingawa madaktari wanasema
kunatofauti kubwa kati ya tembe hizi na zile za kiume ,wakenya wanasitaja kama Viagra
ya wanawake.
Wanawake wanaopata hedhi na
wanaopungukiwa na hamu ya kimapenzi ndio wanakusudiwa kufaidika kutokana na
usiduzi huu.
Kuna hali ya msisimuko kwa
wanawake lakini itakuwa ni muhimu kutumiwa kufuatia ushauri wa daktari kuepuka
madhara ya kiafya yanayosababishwa na matumishi mabaya ya dawa yeyote.
Wataalamu wa tiba hii wa kampuni
ya Sprout Pharmaceticals ambayo tayari inayopatikana Marekani itatibu wanawake wasio changamka
kimapenzi.
Tafiti zinaonyesha kuwa kati ya
wanawake kumi mmoja anakubwa na hali ya kutochangamka kimapenzi.
Mabadiliko ya homoni
mwilini,kutojidhamini, matatizo ya akili na matatizo mengine ya kisaikolojia
yanachagia upungufu wa kuchangamka kimapenzi kwa akina mama.
Kufuatia
uzinduzi huu baadhi ya akina mama niliyowahoji hawajachangamkia au
hawajafurahishwa na hali hii.Wanasema japo litasaidia,itakuwa kwa labda
asilimia 60 lakini kuna haja ya kutafuta suluhu ya kudumu .”hili ni tatizo la
kisikolojia na kuna haja akina mama pia watafute matibabu zaidi kuliko
kutegemea hii tembe pekee yake,alinifahamisha Janet Kavindu ambaye ni mkazi wa
Machakos.
Margaret
Wathoni anasema ni jambo la kutia moyo kwa uvumbuzi huu na atatafuta ushauri wa
daktari ilikujua zaidi,akisisitiza kuwa ni kama vile anautafuta ushauri wa
kiafya anapotaka kutumia dawa za uzazi mpango.
“Nina
raha asana kusikia kuna tiba ya tatizo hili.Nitataka kujua zaidi ili ni chukue
hadua mwafaka kwangu mimi,anasema Wathoni.
Lakini
kuna wanaume ambao wanaona kama temebe hizi ni tatizo kwani sitaleta mchangamko
hadi akina mama wengine waamue kutoke nje ya ndoa.
Muda
tu ndio utaonyesha endapo tembe hii itatatua shida za kimapenzi baina ya
walioko kwenye ndoa na yeyote ule au itakuwa ni tatizo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni