Jumatatu, 7 Septemba 2015

Kenyatta hospital Radiotherapy machine(Cancer)




Image result for kenyatta national hospital radiotherapy machine



Hitilafu ya mashine ya miyale ya umeme (Radio therapy machine)

Mashine inayotumia miyale ya umeme kutoa  matibabu ya saratani na hali duni ya vifaa hivyo katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta yatishia maisha ya wagonjwa wa saratani nchini.

Imekuwa ni hali yakughadhamisha katika hospitali kuu ya kenyatta hapa jijini Nairobi wakati wagojwa wa saratani wanapofika kwa matibabu lakini wanakabiliana na hali ngumu kufuatia upungufu au kuharibika kwa mashine za matibabu mara kwa mara.

Kufuatia hali hii wagonjwa wengi wasio na uwezo wa kutafuta matibabu kwingineko ,huteseka na hali zao kudhoofika wasijue la kufanya.
Image result for kenyatta hospitalGharama ya matibabu katika hospitali hii ya umma ni nafuu ikilinganishwa na hospitali za kibinafsi.

Hata hivyo hospitali ya Kenyatta kupitia wakuu wake wametafuta matibabu hayo katika hosptali za binafsi kwa wagonjwa wanaohitaji matibabu ya dhalura.Lakini swali ni je hali hii inaendelea hadi lini?

Hii si mara ya kwanza au ya pili  kwa vifaa hivyo kupata hitilafu.Miezi mitatu tu, iliyopita wagonjwa walijipata hatarini wakati mashine zilipata hitilafu ,huku mmoja wao wagonjwa akisusia chakula na kujifungo minyororo kwenye kizingiti za mti  nje ya mlango wa matibabu ya dharula.

 Swali ni je hali hii itaendelea hadi lini?

Image result for kenyatta national hospital
Selikali ya kitaifa imetengea hela  sekta ya afya kuhakikisha matibabu yanapatikana bila matatizo katika hospitali zetu .Hata hivyo vifaa vinavyohitajika kwenye hospitali huwa ni vichache au havipo.

Hakika wagonjwa wanahofia kuwa hali hii ikiendelea bila hatua ya kudumu kuchukuliwa au  kurekebisha hali hii,maisha yao yatakuwa hatarini.

Asili mia 80 ya wagonjwa wanaofika Kenyatta kwa matibabu wanatoka mashinani au majimbo,kwa dhana kuwa hospitali ya Kenyatta  hospitali inazo mashine za hali ya juu kiteknolojia ,wala kwa sasa hali si hivyo.
Image result for kenyatta national hospital radiotherapy machine 
Mmoja wa wagonjwa hao ni Mariam ambaye ni mkaazi wa Mombasa na amefika katika hospitali ya Kenyatta kufuatia maagizo ya daktari ,kuwa kila baada ya mwezi inambidi aendelee na matibabu yake.

Lakini la kuhuzunisha ni kuwa alipofika ,alipata habari kuwa matibabu yake hayataendela kama alivyotarajia kufuatia vifaa” kugoma kufanya” kazi..
Kufuatia hali hii hana budi kusubiri hadi mashine zirekebishwe au mpya zinunuliwe.

Hana raha,afya yake imedhoofika na pia ni mchofu kufuatia safari ndefu kutoka Mombasa hadi Nairobi.

Image result for radiotherapy machine kenyattaPia itambidi yeye na wenzake aliyeandamana naye watafute mahali pa kulala ,chakula na mambo mengine ambayo hawakutalajia.Inakuwa ni gharama zaidi kifedha kwani pesa kwake ni adhimu.

Ni jukumu la kila mgonjwa kufuatilia matibabu kama anavyoagizwa na daktari,lakini mara kwa mara  hali  hii inakuwa mbaya wakati mgonjwa analazimika kurudi nyumbani bila matibabu au kusubiri kwa muda mrefu,kutokana na utepetevu wa wahusika wakuu katika wizara za afya au wasimamishi wa hosptali hii.

Maoni

Ni jukumu la serikali kuchukuwa hatua za dharura kurekebisha hali hii ambayo ni ya kughadhabisha katika hospitali kuu ya kenyatta.

Hii ni hospitali inayotegemewa na mamilioni ya wakenya kutoka kote nchini.Kenyatta ni hospitali ya rufaa huku hospitali za majimbo zikiwatuma wagonjwa wanaohitaji matibabu ya dharura Kenyatta,kutokana na ukosefu au upungufu wa vifaa vya matibabu vinavyoabatana na techonolojia ya kiasasa.

Hivyo basi ni jambo la kuhuzunisha kwa wagonjwa na wakenya kwa jumla kuona kuwa tegemeo lao la kupata matibabu limekuwa kama kitendawili au ndoto tu>>

Matibabu ya miale au radiotherapy inahitajika kwa asilimia 80 kwa wanaougua saratani na kila mgonjwa analazimika kulipa shilingi 500 kwa kila wakati anapofika kwa matibabu.

Kusubiri kwa muda mrefu huku ugonjwa ukiendelea kuenea mwilini si jambo la kupendeza.Itapata mgonjwa anaugua lakini kufuatia idadi ya wagonjwa inambidi kusubiri zaidi ya mwaka mmoja au miwili ilianze kupata matibabu.

Hii hupelekea vifo ambavyo vingezuiliwa endapo matibabu ya haraka au wakati ufaao yalitolewa.
Hili ni swala anbalo linastahili dharura maana hapa tunaangazia afya na maisha  ya mwanadamu ambayo ni yadhamana.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni