Flibanserin
Tembe ya kusisimua mapenzi
Wanawake
kupungukiwa na nguvu na hamu ya kufanya mapenzi imekuwa ni jambo ambalo
halizungumziwi kila mahali kwani akina mama wengi wanaliona la aibu.
Lakini
wataalamu wa maswala la afya ya akina mama wanaliona swala la kawaida ambalo
linaweza kurekebishwa kwa matibabu.
Lakini
habari njema ni kuwa vidonge vya kuwaimarishia wanawake hamu au hisia za
kitendo cha ngono imeidhinishwa.Hii ni afueni ambayo itaondoa aibu au kufujika
kwa ndoa kutokana na kutoridhisha waume wao.
Wataalamu
wa afya wanasisitisha kuwa kuna tofauti ya tembe hizi na zile za kiume za
Viagra .
Shirika
moja la Amerika la kuidhinisha na kusimamia dawa liliidhinisha tembe za
Flibanserin kutumiwa kusisimua akina mama kimapenzi baada ya kufanya utafiti na
kupata kuwa tembe hizi ni salama.
Ingawa
madaktari wanasema kunatofauti kubwa kati ya tembe hizi na zile za kiume
,wakenya wanasitaja kama Viagra ya wanawake.
Wanawake
wanaopata hedhi na wanaopungukiwa na hamu ya kimapenzi ndio wanakusudiwa
kufaidika kutokana na usiduzi huu.
Kuna hali
ya msisimuko kwa wanawake lakini itakuwa ni muhimu kutumiwa kufuatia ushauri wa
daktari kuepuka madhara ya kiafya yanayosababishwa na matumishi mabaya ya dawa
yeyote.
Wataalamu
wa tiba hii wa kampuni ya Sprout Pharmaceticals ambayo tayari inayopatikana
Marekani itatibu wanawake wasio changamka kimapenzi.
Tafiti
zinaonyesha kuwa kati ya wanawake kumi mmoja anakubwa na hali ya kutochangamka
kimapenzi.
Mabadiliko
ya homoni mwilini,kutojidhamini, matatizo ya akili na matatizo mengine ya
kisaikolojia yanachagia upungufu wa kuchangamka kimapenzi kwa akina mama.
Kufuatia uzinduzi huu
baadhi ya akina mama niliyowahoji hawajachangamkia au hawajafurahishwa na hali
hii.Wanasema japo litasaidia,itakuwa kwa labda asilimia 60 lakini kuna haja ya
kutafuta suluhu ya kudumu .”hili ni tatizo la kisikolojia na kuna haja akina
mama pia watafute matibabu zaidi kuliko kutegemea hii tembe pekee
yake,alinifahamisha Janet Kavindu ambaye ni mkazi wa Machakos.
Margaret Wathoni
anasema ni jambo la kutia moyo kwa uvumbuzi huu na atatafuta ushauri wa daktari
ilikujua zaidi,akisisitiza kuwa ni kama vile anautafuta ushauri wa kiafya
anapotaka kutumia dawa za uzazi mpango.
“Nina raha asana
kusikia kuna tiba ya tatizo hili.Nitataka kujua zaidi ili ni chukue hadua
mwafaka kwangu mimi,anasema Wathoni.
Lakini kuna wanaume
ambao wanaona kama temebe hizi ni tatizo kwani sitaleta mchangamko hadi akina
mama wengine waamue kutoke nje ya ndoa.
Muda tu ndio
utaonyesha endapo tembe hii itatatua shida za kimapenzi baina ya walioko kwenye
ndoa na yeyote ule au itakuwa ni tatizo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni